Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwana wa Rais Kikwete asema hana ubia na baba yake CCM
Mwana wa Rais Kikwete asema hana ubia na baba yake CCM
By Habari Tanzania | Published  06/11/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu

WAKATI kukiwa na mjadala kuhusu watoto wa vigogo waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, ameliambia Mwananchi Jumapili kuwa, baba yao hakuwahi kuwapa fursa ya kuingilia nafasi za kazi yake.

"Tangu nikiwa mdogo nimeishi na baba na amekuwa akitueleza kuwa hatuna nafasi yoyote ya maamuzi katika kazi yake. Hajawahi kubadilika hata sasa anatueleza kuwa ni yeye aliyechaguliwa na wananchi na sio familia yake," Ridhiwan Kikwete aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

Maelezo haya ya Ridhiwan yanatokana na uamuzi wake wa kugombea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kupitia Wilaya ya Bagamoyo, huku kukiwa na hofu ya kutumiwa nafasi ya baba yake ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM  Taifa ili kupata ushindi.

"Maamuzi haya niliyafanya mwenyewe kwa lengo la kusaka nafasi ya kutoa mawazo yangu katika mikutano ya maamuzi. Nilishangaa kupata simu ya baba akisema kasoma magazeti yakiandika kuwa nagombea NEC.

"NEC ni ngazi kubwa sana na nisingeweza kukimbilia maana inahitaji muda mwingi wa uwajibikaji na pia ingekuwa rahisi kwangu kuhisiwa kuwa natumwa na baba.  Najua ningeweza kushinda pia lakini nisingeweza kufanya kazi vema.

"Nadhani nafasi hii ninayoomba inaweza kuwa nzuri kunilea katika siasa na pia ikinipa fursa ya kufanya kazi ya taaluma yangu ya sheria," alisema.

Kauli ya Ridhiwan inathibitisha ile ya Baba yake aliyowahi kuitoa siku chache baada ya kuchaguliwa na kisha akairudia tena mwaka mmoja baada ya kuwa madarakani.

Kikwete alisema kuwa, urais wake hauna ubia na mtu yoyote na kisha akarudia kusema, wananchi walimchagua yeye na Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein na wengine waliowateua katika nafasi mbalimbali za serikali wamealikwa tu kuwasaidia.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.