Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Azma ya Spika Sitta, wabunge imetimia
Azma ya Spika Sitta, wabunge imetimia
By Habari Tanzania | Published  06/10/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
AZMA ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ya kutaka kuongezwa kwa marupurupu ya wabunge, imetimia.

Ni azma ambayo aliingia nayo katika madaraka aliyonayo, na kwa mara ya kwanza, alijaribu kuitekeleza katika semina maalumu ya wabunge iliyofanyika mwaka jana katika ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Katika semina hiyo, Spika Sitta alieleza nia yake ya kutaka kuboresha mishahara na marupurupu ya wabunge, ili yalingane na wabunge wa nchi zingine za Afrika.

Waandishi wa habari waliokuwa wakihudhuria semina hiyo, waliiandika habari hiyo, na jamii ya Watanzania baada ya kuisoma na kuisikia ikitangazwa katika vyombo vya habari, walipaza sauti kukemea azma hiyo ya Sitta, iliyokuwa ikiungwa mkono na wabunge wengi.

Si siri kwamba, waandishi wa habari waliungana na Watanzania wengine kuwasuta wabunge ambao walikuwa ndio kwanza wanaanza kujiweka sawa kuwatumikia wananchi kama walivyoahidi katika kampeni zao.

Waandishi waliwataka wabunge waache kujifikiria wao binafsi, bali wawafikirie mamilioni ya Watanzania wanaoogelea katika lindi la umasikini, huku wakiandamwa bila kukoma na njaa na matatizo mengine muhimu.

Na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya uchumi, waliwaonya wabunge kuacha kujifananisha na wabunge wa nchi nyingine, ambao uchumi wa nchi zao uko juu. Waliwataka wazingatie hali ya uchumi wa taifa na matatizo yaliyolikabili kabla ya kufikiria kujiongezea kipato.

Spika pamoja na wabunge, hawakufurahishwa na maoni haya, na lawama kubwa walizielekeza kwa waandishi wa habari, kwa kuitangaza taarifa hiyo, walitaka iwe siri.

Baadhi ya wabunge walionyesha kinyongo cha wazi kwa waandishi, na wapo waliodiriki kuomba Spika Sitta awapige marufuku kuhudhuria semina hiyo.

Spika kwa busara zake, ingawa naye alionyesha kinyongo cha wazi kwa waandishi, alifunika kombe ili mwanaharamu apite, akawaacha waendelee na kazi zao.

Ukiwa umepita mwaka mmoja na ushee sasa, tangu sakata hilo lilipotokea, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, ambaye pia ni mbunge, akitangaza mapendekezo ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha kwa Kamati ya Fedha na Uchumi, alikaririwa akieleza kuwa mapendekezo ya bajeti yameonyesha kuwa wabunge wameongezewa sh bilioni 9.3 kwenye posho zao.

Meghji pia aliwatangazia wajumbe wa kamati hiyo kuwa, serikali imeanza kufanya maandalizi ya kuanzisha mfuko wa fedha za kuhudumia majimbo kwa wabunge.

Tunasikitika kusema kwamba, taarifa hizi za uamuzi wa serikali uliotangazwa na Waziri Meghji, zimetushitua na kutushangaza, sababu ni zile zile zilizotushitua na kutushangaza mwaka jana baada ya Spika kutamka kuwa wabunge wanastahili marupurupu na mishahara minono.

Tunausikitikia uamuzi huu kwa sababu wakati serikali ikilia na matumuzi mabaya ya fedha yanayofanywa na watendaji wake, huku ikiwa na mzigo mkubwa wa madeni ambayo ulipaji wake bado ni kitendawili na kwa upande mwingine ikiandamwa na matumizi makubwa kuliko yaliyopitishwa katika bajeti, inathubutu kuongeza marupurupu na mishahara ya wabunge, ambayo mpaka sasa hatusiti kusema kuwa ni ya kiwango cha juu.

Lakini linalosikitisha zaidi, ni kuona kuwa wabunge hawapendi na hawataki masuala yanayohusu maslahi yao kujadiliwa na watu wengine, ila wao wanapenda kujadili masuala ya watu wengine.

Tutafakari pamoja na wabunge wetu, kweli wana haki ya kuibana serikali iwaonyeshe mikataba ya madini yenye utata wakati wao wakiwa hawataki mishahara na marupurupu yao iwekwe hadharani?


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.