Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wateja wa umeme Pemba kuanza kutumia TUKUZA
Wateja wa umeme Pemba kuanza kutumia TUKUZA
By Marshy Abdu | Published  05/29/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Wateja wa umeme Pemba kuanza kutumia TUKUZA
na Saada Said, Zanzibar


WANANCHI wa kisiwa cha Pemba, hivi karibuni wanatarajiwa kuanza kutumia huduma ya umeme wa malipo kabla, unaofahamika kama TUKUZA, baada ya Shirika la Umeme Zanzibar kutangaza kufunga mita za huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi ofisini kwake, Meneja wa huduma za wateja katika Shirika la Umeme la Zanzibar, Abdallah Haji, alisema shirika lao limeagiza mita 20,000 kutoka Afrika Kusini kwa lengo la kuzifunga kwa wateja wa Unguja na Pemba.

“Ni kweli tutafunga mita za TUKUZA kisiwani Pemba huko Wete, ili kuondosha tatizo la usumbufu unaowapata wateja wa shirika,” alisema.

Alisema hadi sasa wameshapokea mita 2,000 ambazo zitafungwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Mradi wa kufunga mita za TUKUZA, ulianza katika mwaka 1999 na kufadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo tayari jumla ya mita 3,900 zimefungwa katika maeneo mbalimbali Unguja yakiwemo Migombani, Michenzani na sehemu za Kiembe Samaki na Uwanja wa Ndege.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.