Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Masumbuko Lamwai asimamishwa uwakili
Masumbuko Lamwai asimamishwa uwakili
By Habari Tanzania | Published  05/27/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Happiness Katabazi


JOPO la majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, limemfungia kufanya kazi ya uwakili, mwanasheria wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Masumbuko Lamwai, kwa kosa la kukiuka sheria za kazi ya uwakili.

Uamuzi wa jopo hilo ulitangazwa juzi na Jaji Juxton Mlay, baada ya kuitupilia mbali rufani ya Dk. Lamwai, aliyekuwa akipinga adhabu ya kumfungia kwa mwaka mmoja kufanya kazi ya uwakili pamoja na kumpiga faini, sh mil 25 iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Mawakili, (Advocate Committee) baada kumkuta na hitilafu za kisheria.

Katika uamuzi huo, jopo lilieleza kuridhia hukumu iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Mawakili na hivyo kutupilia mbali ombi la rufaa namba 18 ya mwaka 2004 iliyowasilishwa na Dk. Lamwai katika Mahakama Kuu.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Mlay alisema kwa niaba ya mawakili wenzake, Jaji Stella Longway na Projestus Rugazia, jopo hili nalo limemfungia Dk. Lamwai kufanya kazi za kisheria kwa muda wa mwaka mmoja kwa sababu hoja 14 zilizopo kwenye rufaa yake hazina nguvu za kuishaiwishi mahakama isimtie hatiani.

“Jopo hili limepitia kwa kina nakala ya hukumu ya kamati na pia hoja 14 za Dk. Lamwai alizoziwasilisha katika rufaa yake, …tumebaini kwamba hoja hizo si za msingi, hivyo jopo hili linatupilia mbali rufaa ya mrufani,” alisema Jaji Mlay.

Awali, Dk. Lamwai alitiwa hatiani na Kamati ya Maadili ya Mawakili baada ya kubainika kutofanya kazi ya uwakili ipasavyo na kumlipa mteja wake, Bernad Mrema sh 25,000,000, aliyekuwa amempa kazi ya kumtetea katika kesi ya madai.

Ilielezwa kuwa, Mrema alimtaka Dk. Lamwai amwakilishe katika madai yake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Inspekta mmoja wa Polisi, kutokana na hasara aliyoipata baada ya gari lake kuzuiliwa katika Kituo cha Trafiki mjini Dodoma.

Kwamba gari hilo lilirejeshwa kwa Mrema likiwa bovu, jambo lililomfanya atafute msaada wa kisheria kutoka kwa Dk. Lamwai ambaye alikubali.

Nakala ya hukumu iliyotolewa na jopo la majaji waliomtia hatiani Dk. Lamwai, inaeleza kuwa Mrema aliendelea kuwasiliana na ofisi ya Dk. Lamwai ambayo hata hivyo, mara kadhaa ilikuwa haifiki mahakamani kumwakilisha.

Inaeleza zaidi kuwa, Mrema aligundua baadaye kuwa Dk. Lamwai alikuwa amesimamishwa kufanya kazi.

Hata hivyo, inaeleza kuwa licha ya Mrema kubaini ukweli huo, Dk. Lamwai aliamua kumpoza kwa kumtafutia wakili mwingine wa kujitegemea, Deo Ringia ili aifanye kazi hivyo.

Wakili Ringia badala ya kuifanya kazi hiyo, alikuwa akimshauri Mrema kujitoa katika kesi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.