Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Anglikana: Aliyemrithi Askofu Dodoma mhaini
Anglikana: Aliyemrithi Askofu Dodoma mhaini
By Marshy Abdu | Published  05/22/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Anglikana: Aliyemrithi Askofu Dodoma mhaini
na Rahel Chizoza


MGOGORO uliolikumba Kanisa la Angalikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), unazidi kuchukua sura mpya kila siku, na sasa kuna tishio la kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya baadhi ya viongozi wa kanisa hilo.

Uongozi wa kanisa hilo ulisema jana mjini hapa kuwa, kanisa halitasita kumfikisha katika vyombo vya sheria, Askofu Msaidizi wa Dayosisi hiyo, Ainea Kusenha, iwapo ataendelea kulivuruga kanisa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu Mkuu wa DCT, Canon Robinson Sangaya, alisema DCT haimtambui askofu huyo kama ni mfanyakazi wake, kutokana na kusimamishwa kazi.

Alisema kitendo cha askofu huyo kuendesha misa katika siku ya Jumapili na kukalia kiti cha askofu katika Kanisa Kuu la Anglikana mjini hapa, hakina tofauti na vitendo vya uhaini.

“Haiwezekani mtu amesimamishwa kazi kwa mujibu wa taratibu na hatambuliki kama mfanyakazi wa DCT, halafu anakwenda kuendesha misa kanisani… ni kinyume cha taratibu pamoja na sheria,” alisema katibu mkuu huyo.

Alisema hivi sasa Kusenha na kundi lake wanafanya kazi ya kuvuruga kanisa, hali ambayo DCT haitaendelea kuivumilia iendelee kutokea katika Kanisa Anglikana.

Hatua hiyo ya kanisa inakuja siku moja tu baada ya Kusenha kutoa kauli wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kusoma misa, kwamba, ataendesha zoezi la kuweka mikono katika parishi zisizomuunga mkono Askofu Mkuu wa DCT, Godfrey Mhogolo.

Katibu Mkuu Sangaya alisema hawataruhusu zoezi hilo lifanyike mahali popote ndani ya dayosisi hiyo, kwani ratiba ya kipaimara imepangwa na DCT na ndiyo inayofuatwa, ambapo Askofu Mhogolo ndiye anayeendesha zoezi hilo katika dayosisi.

Alisema kutokana na Kusenha kuondolewa katika orodha ya wafanyakazi wa DCT, kama anapenda kuendelea kuongoza, anaweza akahamia sehemu nyingine au akaanzisha kanisa lake.

Alibainisha kuwa baada ya kusimamishwa kwake, Kusenha alikata rufaa ambayo aliiwasilisha katika nyumba ya maaskofu na kutolewa maamuzi.

Maamuzi yaliyotolewa na nyumba ya maaskofu ni kwamba wamsamehe deni analodaiwa na wampe uhuru wa kuchagua sehemu nyingine ya yeye kwenda kutumika, ambapo kufuatia taarifa hiyo, walichukua uamuzi wa kumuondoa katika orodha ya wafanyakazi wa DCT.

Sangaya ameitaka jamii kutambua kuwa, hivi sasa Kusenha si mtumishi wa DCT na haruhusiwi kutoa huduma yoyote katika DCT na Kanisa la Angalikana kwa ujumla wake.

“Jana (juzi) tulijua kwamba anaendesha misa, uwezo wa kumtoa tulikuwa nao na nia yake ni kutaka kuchochea fujo kanisani, lakini tulimuacha aendelee maana hatupendi fujo,” alisema.

Sangaya, ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya dayosisi, ambaye amekuwa akifuatilia vikao vyote vya kusimamishwa hadi kuachishwa kazi kwa Kusenha, alisema kikao cha Halmashauri Kuu kiliridhia hatua hizo zilizochukuliwa.

Alisema maamuzi ya kuachishwa kazi kwa askofu msaidizi yalitolewa na halmashauri mwishoni mwa mwaka jana, kwamba kufikia Januari 30 mwaka huu, kama Kusenha angekuwa hajalipa deni analodaiwa, alipaswa kusimamishwa kazi kwa mujibu wa maadili ya dini.

Alisema kilichofanywa na Mhogolo ni kutekeleza maamuzi ya kikao cha halmashauri na baada ya Kusenha kusimamishwa, halmashauri kuu ilikaa kikao Machi 21, mwaka huu na kuridhia kufukuzwa kwake.

Alibainisha kuwa, baada ya kusimamishwa kazi kwa askofu huyo, hakuwahi kuomba msamaha wala kuomba kusamehewa deni, badala yake Askofu Mkuu Donald Mtetemela, ndiye aliyemuombea msamaha.

Alisema kutokana na kuombewa msamaha pamoja na maamuzi kutoka katika nyumba ya maaskofu, halmashauri kuu katika kikao chake iliamua kumuondoa rasmi katika orodha ya wafanyakazi wa DCT.

Alisema kikao hicho kiliridhia kutomfikisha mahakamani, kufuatia madai hayo ya ubadhirifu wa fedha na kutomdai fedha hizo, ambapo walipeleka orodha ya fedha na vitu anavyodaiwa katika nyumba ya maaskofu.

Alisema kwa upande wa suala la ushoga, kikao hicho kilitoa msimamo wa DCT kuwa haitapokea msaada wowote wa hali au mali kutoka kwa kundi au kanisa lolote ambalo limejitangaza kuunga mkono ushoga.

Pia DCT itaendelea kushirikiana na Kanisa la Episcopal la USA kwani halijajitangaza wazi kuwa linaukubali na kuunga mkono ushoga.

Msimamo mwingine ni kuwa DCT haiwezi kukata uhusiano na waumini wa Kanisa hilo la Episcopal la USA, kwani kama wapo mashoga, basi ni asilimia mbili tu ya waumini na hawatambuliwi na kanisa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.