Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Prof. Baregu: Shirikisho EAC si la kuchagua
Prof. Baregu: Shirikisho EAC si la kuchagua
By Marshy Abdu | Published  05/21/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Prof. Baregu: Shirikisho EAC si la kuchagua
na Innocent Mallya


PROFESA Mwesiga Baregu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema uharakishwaji wa Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki, umeingia katika sura mpya baada ya Watanzania kushauriwa kuwa suala hilo ni la lazima na si la kuchagua.

Akizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa kongamano la siku moja lililowashirikisha walimu na wanafunzi wa somo la siasa katika shule za sekondari nchini, Profesa Baregu, alisema hali halisi ilivyo ki-ulimwengu, shirikisho hilo halikwepeki kwa sababu nchi ndogo ndogo za Kiafrika, ikiwemo Afrika Mashariki, hazitaweza ‘kufurukuta’ zenyewe kupambana na changamoto za kiuchumi, kisiasa, na kielimu zinazozikabili.

Alisema Watanzania wanatakiwa wafikie mahali wachangie maoni yao kuhusu shirikisho kwa fikra zaidi kuliko hisia na msisimko, kwani ni suala nyeti litakaloamua mustakabali wa Afrika Mashariki mpya yenye nguvu miaka mingi ijayo.

Profesa Baregu aliishauri serikali kuwa, pamoja na dhamira yake nzuri ya kuheshimu maoni ya wananchi wake katika ukusanywaji wa maoni yao, unaoendelea chini ya kamati ya Profesa Samuel Wangwe, sasa hali inavyoelekea ni bora busara itumike kwa serikali kuwaongoza wananchi na kutoa msimamo wake kwa manufaa ya taifa la sasa na kesho.

“Ninashangaa kuona Watanzania wa leo wanaogopa kujiunga na shirikisho eti tutaambukizwa vita na Rwanda na Burundi. Huu woga unatoka wapi wakati Tanzania hii ndiyo ile ile iliyosaidia kuzikomboa nchi chungu nzima za Afrika miaka ya nyuma?” alihoji Profesa Baregu.

Mariamu Mabodi, ambaye ni mjumbe katika kamati ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu uharakishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, alisema lengo la kongamano hilo ni kuwapa mwanga walimu na wanafunzi hao jinsi ulimwengu wa kisiasa unavyokwenda, ili kupitia mwanga huo waweze kuutumia katika mpango mzima wa zoezi hilo.

Kongamano hilo liliandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali iliyo chini ya walimu wa somo la siasa katika shule za sekondari hapa nchini (CETA) kwa ushirikiano na Asasi ya Konrad Adenauer Stiftung (KAS) ya nchini Ujerumani yenye ofisi zake nchini.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.