Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Gari la waziri kupigwa mnada
Gari la waziri kupigwa mnada
By Habari Tanzania | Published  06/25/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya udalali ya YONO AUCTION MART, inalisaka gari la Naibu Waziri wa Miundombinu, Makongoro Mahanga, aina ya Rav 4 ili ilipige mnada kutokana na deni la mamilioni ya fedha alizokopa kwa rafiki zake.

Habari kutoka ndani ya Kampuni ya Yono, zinasema kampuni hiyo imepewa idhini na mahakama kwa niaba ya walalamikaji wawili ambao wanadai kumkopesha fedha Dk. Mahanga, kabla hajawa na cheo hicho, kwa ajili ya shughuli za kibiashara.

Kwa mujibu wa habari hizo, gari la waziri huyo linalosakwa halionekani mitaani. Makachero wa kampuni hiyo, maarufu kwa kupiga mnada bidhaa za wakopaji wasiolipa, wanahaha kulisaka.

Ofisa mmoja wa Yono ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Yono imekuwa ikilisaka gari hilo kwa muda mrefu. Msako huo ulianza siku chache kabla ya kura za maoni ndani ya CCM mwaka jana, lakini ilishindwa kulitia mbaroni kwa sababu mbili. Kwanza , ni kutokana Dk. Mahanga kuwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge; hivyo hali hiyo ingeweza kuathiri kura zake.

Pili, gari lilifichwa, na Dk. Mahanga mwenyewe alikuwa akitumia teksi na magari ya ndugu na rafiki katika shughuli zake za kampeni.

Chanzo cha Dk. Mahanga kuwa na deni hilo, inadaiwa ni kutokana na msomi huyo kujiingiza kwenye biashara ya ajabu iliyokuwa ikifanywa na watu waliojifanya marafiki zake wa karibu, raia wa nchi jirani za Kenya na wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Inadaiwa kuwa wafanyabiashara hao matapeli mara kadhaa walikuwa wakimfuata Dk. Mahanga wakimtaka awape kiasi cha fedha, nao wakiahidi kurejesha kwa riba kubwa, mara mbili au zaidi ya fedha alizowakopesha, kwa muda mfupi.

“Mara ya kwanza walimwomba awape dola 10,000, (zaidi ya sh milioni 10) aliwapa, wakamrejeshea dola 20,000. Mara nyingine walimwomba dola 40,000, wakarejesha dola 60,000; na mara ya mwisho waliomba dola 100,000 kwa ahadi ya kulipa sh bilioni moja, lakini walipopewa fedha hizo hawakuonekana hadi leo,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Kwa mjibu wa habari hizo, Dk. Mahanga alipoombwa kutoa dola 100,000, alilazimika kukopa kwa marafiki, akafanikiwa kupata fedha hizo anazodaiwa hadi leo.

Mmoja wa watu wanaomdai Dk. Mahanga alikuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini (TRA), Dominiki Olembe (maarufu kwa jina la Kisauti. Mwingine ni mwanasheria wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) aliyejulikana kwa jina moja la Vick.

Tanzania Daima imebaini kuwa gari hilo tayari limeuzwa ili kuepuka adha ya kukamatwa. Lakini yapo madai pia kuwa gari hilo liliuzwa kulipa deni jingine kutoka Benki ya Nyumba, ambako Dk. Mahanga alikuwa akidaiwa mkopo wa nyumba.

Ili kulipa deni hilo , Dk. Mahanga alilazimika kumwandikia barua aliyekuwa Spika wa Bunge, Pius Msekwa, akimwomba amlipe mapema kiinua mgongo chake cha miaka mitano ili alipe madeni hayo, lakini alikataliwa.

Akizungumza na Tanzania Daima, Dk. Mahanga alikiri kuwa na deni hilo lakini akasema ni la muda mrefu na tayari alikuwa ameshamalizana na wadeni wake.

“ Kwanza ninyi habari hii mmeipata wapi? Lakini mimi najua habari hii inaletwa na kundi la watu niliogombea nao kwenye uchaguzi. “Lakini mtafute Olembe umuulize kama bado ananidai; mfuate mtu mwingine uone kama kweli bado ananidai,” alisema.

Alisema yeye si tapeli kiasi hicho, lakini aliwahi kutapeliwa na watu wa aina hiyo, akasisitiza kuwa suala hilo alishalimaliza muda mrefu.

Mbali ya kuwatuhumu washindani wake kisiasa aliogombea nao ubunge kwa kutoa taarifa hiyo, Dk. Mahanga alienda mbali zaidi na kumtuhumu mmoja wa mawaziri wenzake, ambaye amebadilishwa wizara katika awamu hii, kwamba anahusika katika kumchafulia jina ili aonekane hafai.

“Jambo hili si geni, linajulikana, hata mkiandika, unafikiri Rais Kikwete atanifukuza kwenye nafasi hii?” alihoji Dk. Mahanga.

Hakufafanua kwa undani suala hilo , bali alitumia muda mwingi kumshutumu mwandishi wa habari hizi na kumtisha kwamba atakwenda mahakamani kuishitaki Yono na Tanzania Daima, kwa madai kuwa suala hilo lilikwisha kumalizika


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.