Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Migomo ya walimu yaibuka tena sekondari Vituka
Migomo ya walimu yaibuka tena sekondari Vituka
By Marshy Abdu | Published  05/18/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Migomo ya walimu yaibuka tena sekondari Vituka
na Tamali Vullu


WALIMU 26 wa Shule ya Sekondari Vituka, Dar es Salaam, jana waligoma kufundisha na kusimamia mitihani ya majaribio (mock) ya kidato cha pili na nne shuleni hapo kwa madai ya kutolipwa mishahara.

Akizungumza na gazeti hili shuleni hapo kwa niaba ya walimu wenzake kwa masharti ya kutotajwa jina, mmoja wa walimu hao alisema mpaka sasa hawajalipwa mishahara ya Aprili bila kuwapo kwa maelezo ya kutosha kutoka kwa uongozi wa shule.

Alisema Ijumaa iliyopita walikaa na uongozi wa shule hiyo na kuahidi kuwalipa fedha hizo, lakini hadi juzi jioni mkuu wa shule hiyo alikuwa hajawaeleza chochote kuhusu suala hilo na ndipo jana walipoamua kugoma.

“Kutokana na hali hiyo, tukaweka msimamo kuwa hatutafanya kazi yoyote ya kitaaluma mpaka tutakapolipwa mshahara. Awali, walimu waliokuwa wasimamie mitihani waligoma kuungana nasi, lakini tuliwashawishi mpaka wakakubali,” alisema mwalimu huyo.

Alieleza kuwa jana walipogoma kuingia darasani na kusimamia mitihani hiyo, Mkuu wa Shule hiyo, Albert Mwaipopo, alifika shuleni hapo na kwa kutumia lugha ya vitisho, aliwataka walimu waliokuwa zamu kusimamia mitihani kufanya hivyo, vinginevyo wangefukuzwa kazi.

Hata hivyo, walimu hao hawakutii amri hiyo, na ndipo alipowataka mmoja wao kuingia naye ofisini kwa mazungumzo zaidi.

“Baada ya mazungumzo ya muda mfupi na mwakilishi wetu, Mkuu wa Shule ametuahidi leo (jana) jioni kutupatia mshahara wetu, hivyo tumesitisha mgomo na walimu sasa wanafundisha na wanafunzi walianza kufanya mitihani saa 3:45 badala ya saa 2:00,” alisema.

Mwalimu huyo alieleza kuwa iwapo mkuu huyo wa shule hatatekeleza ahadi hiyo, leo wataendelea na mgomo hadi watakapopatiwa haki yao hiyo.

Aliongeza kuwa tangu mwalimu huyo alipoingia shuleni hapo Mei mwaka jana, wamekuwa wakipata taabu katika suala la mishahara na kwamba Machi mwaka huu shule hiyo ililazimika kukopo fedha kutoka Shule ya Sekondari Tegeta kwa ajili ya kulipia mishahara ya walimu.

“Shule hii kwa mwaka inaingiza zaidi ya sh milioni 250, na karibu wanafunzi wote wamelipa ada. Tunashindwa kuelewa kwa nini wanashindwa kutulipa mishahara yetu kwa wakati. Sasa tumeamua kuweka silaha chini, kwani hali imekuwa ngumu,” alisema.

Mbali na suala la mishahara, pia wanadai kuwa hawalipwi fedha za nauli, posho mbalimbali na pia hawapelekwi katika semina za mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiongezea ufahamu.

Wakati gazeti hili lilipokuwa shuleni hapo kufuatilia hali hiyo, Mwaipopo hakuwepo ofisini kwake.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mkuu wa Shule hiyo, Mwaipopo, alisema kuwa walimu shuleni hapo hawakugoma, kwani wanaendelea na kazi kama kawaida.

“Hakuna mgomo wowote. Walimu wote wameingia darasani na waliokuwa na zamu ya kusimamia mitihani wamefanya hivyo,” alisema Mwalimu Mwaipopo.

Hata hivyo, alikiri kuwapo kwa madai ya mishahara na kusema kuwa walimu hao watalipwa kulingana na shule hiyo itakavyopata fedha.

“…leo benki hawajatoa fedha. Siwezi kufahamu lini tutapata fedha za kuwalipa mishara. Hiyo itategemea na mapato ya shule, kwani kuna mahitaji mengi zaidi ya mishahara,” alisema mwalimu huyo na kukata simu.

Shule hiyo ipo chini ya Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.