Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mrema kuunda tume ya kumhoji Prof. Mukandala
Mrema kuunda tume ya kumhoji Prof. Mukandala
By Marshy Abdu | Published  05/18/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Mrema kuunda tume ya kumhoji Prof. Mukandala
na Chalila Kibuda na Safina Tibanyendela


MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Agustine Mrema, amesema amepanga kuunda tume itakayomhoji Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala, kuhusiana na tuhuma za kukivuruga chuo hicho.

Akizungumza na Tanzania Daima jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mrema alisema kuwa matatizo yaliyokikumba chuo hicho siku chache baada ya kukabidhiwa madaraka ya kukiongoza, yamedhihirisha kuwa Mukandala hana uwezo wa kukiongoza chuo kikuu.

Akiizungumzia tume hiyo, alisema kuwa yeye ndiye atakuwa mwenyekiti wake, na watamfuata kumhoiji Mukandala kwa kina kuhusiana na sakata la kusimamishwa kwa wanafunzi na migomo chuoni hapo.

Alisema baada ya kumaliza kumhoji Profesa Mukandala, tume yake itatoa taarifa kwa umma kuhusiana na mahojiano hayo.

Mrema alimtaka Mukandala kuendesha chuo kikuu kama taasisi ya elimu ya juu ambayo inapania kutoa viongozi wa baadaye wa taifa.

Mrema alidai kuwa mgogoro unaoendelea hivi sasa UDSM umekuzwa bila sababu za msingi na uongozi wa chuo na serikali kwani kiasi cha fedha ambacho wanafunzi walikuwa wanakihitaji ni kidogo mno ukilinganisha na hasara ambayo taifa limepata kutokana na kusimamishwa kwa masomo chuoni hapo kwa takriban mwezi mmoja.

Wanafunzi hao waligoma wakiitaka serikali iwapatie ufadhili wa gharama za masomo kwa asilimia 100, badala ya asilimia 60 inayoitoa hivi sasa kupitia Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.