Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Viongozi wa serikali sasa kujieleza CCM
Viongozi wa serikali sasa kujieleza CCM
By Habari Tanzania | Published  05/17/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Rahel Chizoza, Dodoma


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeanzisha utaratibu mpya wa kuwaita watendaji wa serikali kutoa taarifa za kiutendaji za serikali katika vikao vya Halmashauri Kuu ya chama hicho.

Akiongea na waandishi wa habari mjini hapa jana, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, alisema lengo la hatua hiyo ni kuwawezesha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kufahamu ni kwa kiasi gani ilani ya uchaguzi ya chama hicho inatekelezwa na watendaji wa serikali.

Makamba alisisitiza kuwa kipimo pekee cha kuona jinsi ilani ya uchaguzi ya CCM inavyotekelezwa katika Awamu ya Nne ni kupokea taarifa na kuona mafanikio yaliyofikiwa katika malengo ya kuleta maendeleo ya nchi katika kipindi hicho.

Makamba alisema katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika mwanzoni mwa wiki na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, jumla ya taarifa saba za serikali, ziliwasilishwa na kujadiliwa na kamati hiyo.

Mojawapo kati ya taarifa zilizowasilishwa ni taarifa ya mpango wa kuingiza shule za sekondari wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2006, ambapo taarifa hiyo ilionyesha kuwepo kwa mafanikio kwa asilimia 89.

Alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo ya elimu katika kipindi cha miezi sita, jumla ya shule 1,040 za sekondari zimejengwa nchini kote na kuwawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wamefaulu na kukosa nafasi ya kuendelea, kupatiwa nafasi za masomo.

Alisema wanafunzi waliofaulu darasa la saba ni 468,252, lakini waliopata nafasi kwa mujibu wa shule zilizokuwapo wakati huo ni 235,905. Hali hiyo iliifanya serikali kuandaa utaratibu maalumu wa kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapatiwa nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Alibainisha kuwa mwaka 2005, wakati Serikali ya Awamu ya Nne inajiandaa kuingia madarakani, kulikuwa na shule za sekondari 1,202 nchi nzima, lakini kwa kipindi cha miezi 18 tangu serikali hiyo ishike hatamu, kumekuwapo na ongezeko la shule 2,269 na kufanya jumla ya shule za sekondari nchini ifikie 3,471.

Makamba alisema sambamba na ongezeko hilo la shule za sekondari, kumekuwa pia na ongezeko la walimu ambapo jumla ya walimu 6,668, sawa na asilimia 68.95, walipatiwa ajira mpya, ambapo serikali inaendelea na mpango wa dharura wa kuajiri walimu wapya 3,305 ili kutimiza malengo iliyojiwekea.

Kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Makamba alisema kitaanza Septemba mwaka huu na kitadahili wanafunzi 1,000, ambapo idadi hiyo itaongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia wanafunzi 40,000 ambao wamekusudiwa kujiunga.

Alisema hivi sasa miundombinu ya kuanzia katika chuo hicho ipo tayari, sanjari na uongozi wa chuo, ambapo alibainisha kuwa vikao vya CCM havitakuwa vikifanyikia katika ukumbi wa Chimwaga kwa sasa, badala yake vitafanyikia kwenye kumbi nyingine.

Halmashauri Kuu ya CCM pia ilipokea taarifa ya mapinduzi katika kilimo ambayo ilibainisha kuwa jumla ya sh trilioni 2.5 zitatumika katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini katika kipindi cha mwaka 2006/2007 hadi 2012/2013.

Kupitia mpango huo wa mapinduzi ya kilimo, wananchi watawezeshwa kutumia zana za kisasa zaidi katika kilimo hivyo kuzalisha zaidi na kuondokana na tatizo la uhaba wa chakula.

Makamba alisema kuwa kwa mujibu wa mpango huo, kiwango cha eneo lililo chini ya kilimo cha umwagiliaji kitaongezwa kutoka hekta 250,000 hivi sasa na kufikia hekta milioni moja ambazo zitawawezesha wananchi kuzalisha hata kama hakuna mvua za kutosha katika msimu wa kilimo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by hp)
    Rating
    Viongozi wa serikali wajieleze bungeni kwani hiyo ndiyo taasisi wanayotakiwa kujieleza kisheria. CCM siyo bunge.
     
Submit Comment


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.