Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ujenzi daraja la Malagarasi washika kasi
Ujenzi daraja la Malagarasi washika kasi
By Marshy Abdu | Published  05/16/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Ujenzi daraja la Malagarasi washika kasi
na Amana Nyembo


MPANGO wa ujenzi wa daraja katika Mto Malagarasi mkoani Kigoma, sasa unaonekana kushika kasi kufuatia kuwasili nchini kwa watalaamu wanane kutoka Korea Kusini kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi wa daraja hilo ambao umekuwa ukizungumziwa kwa muda mrefu kama mkakati wa kuunganisha Mkoa wa Kigoma na Mkoa wa Tabora, utagharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 25.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Daniel Nsanzugwanko, alisema ujenzi huo ni matokeo ya ziara iliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete huko Korea Kusini.

Alisema katika ziara hiyo, rais alifanikiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi alipotembelea Korea kwa ajili ya kutafuta fedha ya ujenzi huo.

Nsanzugwanko alisema ujenzi utaanza mara baada ya maandalizi yote kukamilika kwa kuwa mpaka sasa hatua za kiutendaji, kama sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo, tayari zimeshaanza.

Alisema kuwa wahandisi wametoa siku 90 kwa ajaili ya maandalizi kabla ujenzi wa daraja hilo haujaanza.

“Moja ya ilani ya CCM ilikuwa ni mradi wa ujenzi wa daraja wa Mto Malagarasi, ambao unagawa mikoa miwili, yaani Tabora na Kigoma, lakini hata hivyo utekelezaji wa ilani ni wa wote, kwa wanachama na wasio wanachama,” alisema Nsanzugwanko.

Alisema timu hiyo ya wahandisi juzi ilikuwa Hazina kwa ajili ya kujadili ujenzi huo, jana ilikuwa Wizara ya Miundombinu na leo itakuwa ziarani katika Mkoa wa Kigoma kuangalia eneo la Mto Malagarasi katika eneo litakapojengwa daraja hilo pamoja na kukutana na maofisa wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani humo.

“Mpaka sasa Wakorea wameonyesha kuwa wapo tayari katika kufanya kazi hii ya ujenzi wa daraja na naamini itakuwa hivyo kwa kuwa wametoka katika kampuni kubwa,” alisema Nsanzugwanko.

Pamoja na kuwa na wahandisi kutoka nje ya nchi, Nswanzugwanko alisema makandarasi na wahandisi wa hapa nchini nao watapata fursa ya kushirikiana na wageni na hiyo itakuwa ni fursa nzuri kwao kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na ujenzi hasa wa madaraja.

Alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo ni hatua muhimu katika kufungua uchumi wa Mkoa wa Kigoma, ambao kwa muda mrefu umekuwa ukikwazwa na ubovu wa miundombinu ya usafiri.

Aidha, alisema daraja hilo litakuwa ni kichocheo cha biashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kupitia Mkoa wa Kigoma.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.