Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wapinzani waweka msimamo
Wapinzani waweka msimamo
By Habari Tanzania | Published  05/10/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Irene Mark


VYAMA vinne vya siasa vya upinzani nchini, vimekubaliana kimsingi kuwa na msimamo wa pamoja katika kudai na kutetea masilahi ya wananchi dhidi ya serikali kabla ya kufikiwa kwa ndoto ngumu ya kuunda chama kimoja.

Makubaliano hayo yatatiwa saini leo na wenyeviti wa vyama hivyo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari. Vyama vilivyopo kwenye muungano huo ni CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbord Slaa, alisema mchakato unaoendelea sasa ni kuhusu namna ya vyama hivyo vitakavyoshirikiana katika masuala mbalimbali ya kisiasa.

Alisema lengo la vyama hivyo hivi sasa ni kuunganisha nguvu katika kushinikiza madai kuhusiana na masuala ya kimaendeleo na kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa kinyume cha utaratibu serikalini kwa masilahi ya wananchi wote.

“Kuna confusion kubwa katika uelewa wa muungano huu… kinachofanyika kwetu ni kuungana na kuimarisha umoja huu ambao utakuwa kwa masilahi ya Watanzania wote.

“Kupitia muungano huu tutashinikiza mabadiliko ya katiba, maboresho ya sheria ya rushwa, uchaguzi huru na haki, kutetea wanachuo waliosimamishwa masomo kuhusu asilimia 40 na mambo mengine.

“…Tunafanya yote haya kwa ajili ya wananchi, sasa hao wanaosema tunaunda chama kimoja sijui wanapata wapi maneno haya,” alisema Dk. Slaa na kuongeza kuwa hakuna mpango wa kuua vyama hivyo bali ni kuimarisha umoja wa kisiasa.

Kadhalika, Dk. Slaa alisisitiza ukaribu wa vyama vya siasa nchini na kusema umoja ni nguvu, hivyo ili kuikosoa serikali kwa hoja nzito, wameona umuhimu wa kuwapo kwa muungano huo.

Alisema umoja wao utaamsha uwajibikaji wa watumishi serikalini na utekelezaji wa haraka wa ahadi zilizotolewa, pia kuleta mageuzi ya kisiasa, uchumi na kijamii kwa maendeleo ya Tanzania.

Kadhalika, Dk. Slaa alisema kwa sasa, ni mapema mno kuunganisha vyama hivyo kutokana na ukweli kuwa kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya vyama hivyo, sheria za nchi na kuvunja haki za wanachama wao.

“Unajua hayo yanayosemwa sasa ni uvumi, lakini sisi kama vyama tuna katiba, kanuni na sheria zetu, hivyo kabla ya kuungana lazima tuzingatie haki za wanachama wetu na kupitia upya katiba za vyama vyetu,” alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa muundo wa chama kimoja kutoka muungano huo, utatokea baada ya mchakato utakaochukua muda mrefu, utakaozingatia haki, usawa na wajibu wa vyama na wanachama wao.

Dk. Slaa alibainisha kuwa hakuna ndoto za kufanya hivyo na hata zikitokea itachukua muda mrefu kuafikiana kuhusu kuunda chama kimoja.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.