Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Amina Chifupa kulipua bomu leo
Amina Chifupa kulipua bomu leo
By Habari Tanzania | Published  05/7/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu


MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), amesema leo analipua bomu mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuvunjika ndoa yake na Mohamed Mpakanjia, tukio analosema limesababishwa na kiongozi mmoja ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni Naibu Waziri.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Amina, alisema anamuomba Mwenyezi Mungu amuamshe salama, ili aweze kuzungumzia suala hilo ambalo anafahamu kuwa linaweza kumuweka katika wakati mgumu kabisa.

“Nafahamu ninapambana na watu hatari, lakini kesho (leo) namuomba Mwenyezi Mungu aniamshe salama, ili niweze kuliweka bayana suala hili mbele ya waandishi wa habari MAELEZO. Nimekusudia kusema ukweli wote kuhusu suala langu,” alisema Amina.

“Daima nasimamia ukweli na sababu ya dhamira yangu. Nipo tayari kufungwa au kuchukuliwa hatua yoyote iwapo nitaonekana sina nidhamu… hata ikibidi kupoteza ubunge na uanachama wangu wa CCM. Mimi si mwanasiasa wa ‘ndiyo mzee’,” alisema Amina baada ya kuulizwa iwapo ukweli anaotaka kusema hautamgharimu.

Amina ambaye ameihakikishia Tanzania Daima kuwa alipewa talaka na mumewe, Mei 3 mwaka huu, anasema tukio hilo lilikuja baada ya kiongozi huyo wa CCM ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho kumuita mumewe ofisini kwake.

“Nilipewa talaka siku ile ile baada ya Mpakanjia kutoka ofisini kwa kiongozi huyo. Kwa kweli (anamtaja) ndiye aliyevunja ndoa yangu kwa kumuambia mume wangu mambo ya uongo,” alisema.

Habari zaidi ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kwamba, Amina anaamini kwamba kikubwa kilichosababisha akutwe na masahibu hayo, ni kile kinachoelezwa kuwa uamuzi wake wa kutaka kugombea uenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), hatua ambayo inaonekana kuwashtua na kuwakera baadhi ya viongozi wa sasa wa umoja huo.

Hivi sasa Mwenyekiti wa UVCCM ni Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana anayetarajiwa kumaliza kipindi chake mwakani.

Hata hivyo, Amina alipotakiwa kueleza iwapo alikuwa akikusudia kugombea nafasi hiyo, hakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kumtaka mwandishi kusubiri hadi wakati utakapofika kwani kuna muda mrefu bado, kabla ya yeye kufikia uamuzi huo.

Mbali ya hilo, Amina alielezwa kushangazwa kwake kuona masuala yake ya ndoa, yakipelekwa bungeni, wakati mahusiano yake ya nyumbani hayana uhusiano wowote na ubunge wake au uanasiasa wake.

Habari ambazo zilithibitishwa zinaonyesha kuwa, Amina amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbunge kijana wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambaye alipopigiwa simu na gazeti hili jana, aliyapuuza madai hayo ambayo alisema; “hayana ukweli.”

Zitto mmoja wa wabunge machachari wa upinzani, alisema anafahamu kwamba suala hilo limeandaliwa na kundi la watu wenye sababu za kisiasa, ambao wamekuwa wakimtafuta yeye na Chifupa kwa muda mrefu.

“Ukaribu wangu na Amina ni wa kikazi tu… na ukaribu huo ulianza siku Spika wa Bunge alipotuteua tuhesabu kura za wabunge zilizomuidhinisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Siku hiyo tulipokuwa tukihesabu kura, afisa mmoja wa bunge alitufuata katika chumba cha kuhesabu kura na akatutaka kutozitaja kura mbili zilizokuwa zimeharibika, jambo ambalo mimi na Amina tulilikataa. Tangu hapo nilianza kumheshimu Chifupa baada ya kubaini kuwa alikuwa mtu makini na mwenye msimamo. Tangu wakati huo tumekuwa na uhusiano wa karibu kikazi,” alisema Zitto, alipohojiwa kwa njia ya simu.

Alisema, siku zote amekuwa na uhusiano mzuri na wabunge wote vijana kwa wazee, lakini anashangazwa na uvumi juu ya uhusiano wake na Amina kuonekana vinginevyo.

Gazeti moja la kila siku, (si Tanzania Daima), jana lilimkariri Mpakanjia, akithibitisha kumtaliki mkewe baada ya kubaini ndoa yake ikiingiliwa na mbunge wa CHADEMA ambaye hata hivyo hakumtaja.

Habari zaidi ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kwamba, ushahidi mkubwa unaoonekana kuwaunganisha kimapenzi wabunge hao vijana, ni tukio la siku moja jioni, ambalo Amina alionekana akiwa amevaa koti la Zitto, wakiwa wameketi pamoja katika Hoteli ya Dodoma.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by mwanamu rashidi)
    Rating
    Nudgu muandishi madai niliyoyasoma kuhusu kutalikiwa kwa mheshimiwa amina chifupa ni kitu cha kawaida kuolea na kuachika wala yeye si kwanza. Isipokuwa tu wamezidi kumuandama na pia huyo mheshimiwa ambaye ametajwa hapo juu ameona wivu tu kwa amina kutaka kuwania uenyekiti wa vijaya sasa yeye atakaa mpa lini wa kati muda wake unamalizika mwaka ujao. Aibu sana kumvunjia mtu ndoa yake bila ya sababu mbona wanandoa wengi si wanawake na wanaume wanafanya hayo mambo vipi kwake imekuwa kioja chakumtilia chonjo hadi aachike kwa kutumia mambo ya uwongo na aibu tu ya kumfedhesha huyu amina. Naomba sana rais kikwetu angalie hili swala kwa undani ili ampige msasa huyu fitna hasidi mkubwa ajirekebishe kuchaguliwa kuwa pale kama mwenyekiti wa vija taifa na waziri mdogo sio tija au warrant ya kukaa pale maisha kama wlipovikuwa wanafanya ukiritimba wa kutowachikia madaraka hii ni utawala wa kasi, ari na nguvu mpya acheni roho mbaya za kichawi.
     
  • Comment #2 (Posted by Peter Maiga)
    Rating
    Amina na Zito wamejitetea we lakini za mwizi arobaini!!
    Wewe mtu si mume wako unafikiaje hatua ya kuvaa koti lake?watu wakueleweje?Acha ujinga sawa?sema kweli minatoa ukubali kwamba yasemwayo yamefanyika.
     
  • Comment #3 (Posted by Godlove)
    Rating
    Namuona Mpakanjia kuwa mpuuzi na asie na misimamo. Mtu unawezaje kuendesha ndoa kupia ushauri? Acha amtariki ili wanaojua thamani ya Amina wachukue nafasi hiyo adimu.
     
  • Comment #4 (Posted by sufian ngenzi)
    Rating
    Nimesoma kwa kuchelewa stori hii. Hata hivyo naungana nayo kama ifuatavyo, Bw Mpakanjia alikuwa sahihi kumtaliki Amina kutokana na vituko vya Amina na Zitto walivyokuwa wakifanya Bungeni. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMIN.
     
  • Comment #5 (Posted by JAKINDA CHAPOMBE)
    Rating
    Huyo anayejiita Mwenyekiti UVCCM,Emanuel Nchimbi,Mtu mzima ovyo,kama wewe ulitaka kutumia cheo chako cha Uenyekiti UVCC na Unaibu waziti wako,Kumtongoza marehemu
    Amina ambaye alikukataa,ilikweje umfuate Mpakanjia kwenda kutoa umbea,je wewe hujawahi kutemebea nje ya ndoa,hii inaonyesha kuwa hata amina angekukubali wewe ungekuja kumpakazia kuwa ni malaya,nafikiri hata yeye marehemu alijua kuwa wewe huna msimamo na ni mbea ndiyo maana alikukataa,
    Vilevile,Umejiaibisa kitaifa,kisiasa,hata kwenye familia yako sababu sasa hivi hakuna siri inajulikana kuwa wewe ndiyo chanzo cha haya mambo yote kutokea,Sielewi mke wako au ngugu zako wanalichukuliaje suala hili la wewe kmfuata mpakanjia na kumwambia umbea huo uliomletea matatizo makumbwa marehemu na fedheha,Kama mimi ningekuwa mke wako,ningekuuliza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutaka kujua kuwa,wewe sio ndugu wa mpakanjia labda kama umeutafuta undugu na kujenga urafiki naye kwa lengo la kumchafua amina,imekuwaje uumie sana hata kama kweli alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake?Hapa kuna sababu mimi ni mtu mzima na mtu mzima hadanganywi na pipi hata siku moja ,wewe kuna uhakika kuwa ulimtongoza huyo marehemu na baada ya kukutolea nje,ulimuonea wivu huyo aliyekuwa naye karibu,vilevile ulimuonea wivu pale alipojitangaza kugombea nafasi ya uenyekiti UVCCM,Ndio ukaamua kumchafua kwa style hii.Wewe unataka ushike nafasi ngapi?UVCCM wewe ingawa ndio unaachia ngazi unaibu waziri wewe,hayakutoshi kama ni kutaka kuwa karibu zaidi na rais mbona wewe kama naribu waziri ni mtendaji wake mkubwa na una nafasi nzuri ya kuwa naye rais karibu?Hapa kuna lako jingine tu,fitina chuki na wivu,Jua kuwa kama siku ile amina angelipua bomu mambo yako yote uliyomfanyia ambayo bado ni siri na fumbo kwa wananchi yangejulikana,NA mimi nina endelea kukuambia kama marehemu alivyokwambia kuwa malipo ni hapahapa duniani!!leo amina amefariki,je huoni kuwa hata wewe unaingia katika idadi ya waliosababisha kifo chake?Je unajisikiaje kama wewe ni binadamu,kuwa ahkuna cha zaidi ulichopata uenyekiti uvccm utaacha...umefaidika na nini?Nauhakika huko aliko amina sasa anaenedelea kukuombea ili malengo yako yaenedelee kutimia sawa bwanamkubwa!
    Ila mimi nakuonya kuwa usirudie tena kuwafanyia hivi watu wengine huyo amina familia yake wametulia..ingekuwa familia nyingine ambayo inajua kabisa wewe ndio uliyesababisha haya matatizo kuanza hadi yakamletea mauti wasingekubali....Ni lazima,uungame na uombe mungu akusamehe kwa hili,na kabla hujaomba msamaha wa nmungu ningekushauri uende kwenye kaburi la Amaina lupembe ukagalegale umuombe msamaha.Bila hivyo kitendo hicho kitakusononesha na kukupa mawazo mengi kila siku ya maisha yako!!!!Kwa heri.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.