Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wasomali sasa tatizo
Wasomali sasa tatizo
By Habari Tanzania | Published  05/4/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Charles Ndagulla


WIMBI la raia wa Somalia wanaokamatwa nchini, linazidi kuongezeka kwani katika wiki mbili zilizopita, jumla ya Wasomali 199 wamekamatwa katika mikoa mitatu tofauti.

Idadi hiyo imefikia baada ya Wasomali 58 kukamatwa mpakani mwa Tanzania na Kenya katika Kijiji cha Kahe Kyomu, wakiwa wamefungiwa ndani ya nyumba ya mwananchi mmoja.

Inadaiwa kuwa, Wasomali hao wanapita tu nchini kuelekea nchi za Kusini, wakikimbia mapigano ambayo yamepamba moto nchini kwao.

Katika tukio hilo la juzi, Wasomali hao 58, walikutwa wakiwa wamechoka na kudhoofu kutokana na safari ndefu ya miguu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Musa Samizi, aliiambia Tanzania Daima jana ofisini kwake kuwa, msamaria mmoja alipiga simu ofisini kwake kumjulisha kuwepo kwa kundi hilo la wahamiaji haramu.

Aliongeza kuwa, baada ya kupokea simu hiyo, aliwajulisha maofisa wa usalama wa taifa ambao walielekea eneo hilo mara moja. Walifanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji hao haramu, lakini mmiliki wa nyumba hiyo, akitimua mbio kukwepa mkono wa dola.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ngh’oboko, alithibitisha kukamatwa kwa raia hao wa Somalia alipozungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake na kuongeza kuwa, wanatoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Alisema miongoni mwa watu hao, 48 ni wanaume na 10 ni wasichana wenye umri mdogo. Kamanda huyo alidai kuwa, watu hao walikusanywa na kusafrishwa kutoka nchini humo na watu weusi.

Alifafanua kuwa, katika maelezo yao wakati wanahojiwa, Wasomali hao walisema kuwa walisafirishwa na ‘Waswahili’ ambao waliwahadaa kuwa watawatafutia hifadhi ya ukimbizi katika nchi za Ulaya.

Aliongeza kuwa, baada ya kuvuka mpaka kutoka nchini Kenya na kuingizwa katika nyumba hiyo inayomilikiwa na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Evanko Kessy, walijikuta wapo peke yao bila kuona mwenyeji wao hadi walipotiwa mbaroni.

Hata hivyo, kamanda huyo wa polisi amekiri kuwepo na ugumu wa kuudhibiti mpaka wa Tanzania na Kenya kutokana na ukubwa wake na wingi wa ‘njia za panya’ zinazokadiriwa kuwa zaidi ya 360, ambazo zina uwezo wa kupitisha magari.

“Mpaka wetu ni mkubwa mno, hatuwezi kuulinda wote kwa kutawanya polisi kila mahala, ni mkubwa sana, umesambaa hadi Longido,” alisema alipotakiwa kuelezea hatua zinazochukuliwa kakabiliana na wimbi hilo la wahamiaji haramu.

Aidha, kamanda huyo alitoa wito kwa raia wema wenye taarifa sahihi juu ya Watanzania wanaoshirikiana na raia wa Kenya kuwasafirisha wahamiaji haramu kwa ujira mnono wa wastani wa dola 300 hadi 350 kwa kila mhamiaji mmoja, kuifahamisha polisi.

Pamoja na kuthibitisha kukamatwa kwa watu hao, kamanda huyo hakuwa tayari kutoa orodha ya majina yao kwa vyombo vya habari na kudai kuwa, wanaendelea kumsaka mmiliki wa nyumba walimokutwa Wasomali hao.

Baadhi ya Watanzania waishio mpakani katika maeneo ya Makuyuni, Kilototoni, Chekereni, Kahe Kyomu na maeneo mengine, wanadaiwa kujihusisha na biashara hiyo haramu, huku wakidaiwa kushirikiana na polisi wa doria katika mji mdogo wa Himo.

Mmoja wa raia hao waliokamatwa, ambaye ni msichana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 15, bila kutaja jina lake, alisema kuwa wamekimbia risasi na mabomu yanayozidi kurindima kila kukicha nchini mwao.

Akizungumza kwa tabu lugha ya Kiswahili, msichana huyo alidai kuwa walikuwa wameingia nchini wakiwa njiani kuelekea Malawi kwa lengo la kutafuta ajira.

Hili ni tukio la tatu katika siku za hivi karibuni ambapo katika tukio la kwanza, Wasomali 99 walikamatwa mkoani Mbeya, wakiwa wamejificha ndani ya lori, kando kando ya Mto Songwe.

Taarifa iliyotolewa na polisi mkoani humo ilisema kuwa Wasomali hao walikuwa njiani kuelekea Malawi na Afrika Kusini.

Aidha, baadhi ya Wasomali hao walikutwa wakiwa na hali mbaya na wengine walilazwa hospitali kufuatia kuugua ugonjwa wa kuhara.

Wasomali hao tayari wameshasomewa mashitaka ya kuingia nchini bila vibali isipokuwa mmoja ambaye ilishindikana kumsomea kutokana na hali yake kuwa mbaya hospitali alikolazwa.

Aidha, mapema wiki hii, wahamiaji haramu wengine 42 walikamatwa katika Kijiji cha Mkurunge huko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Kati ya watu hao, 24 walitambuliwa kuwa ni raia wa Ethiopia na waliosalia ni Wasomali.

Tukio hilo la Moshi linakuja siku moja baada ya gazeti moja la kila siku kuripoti kuwa, hali ya ulinzi katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Sirari mkoani Mara si nzuri kwani mpaka huo unalindwa na kampuni binafsi ya ulinzi.

Aidha, tukio la kukamatwa kwa Wasomali hao 58 juzi, limekuja wakati serikali ikieleza kuwa imeweka ulinzi wa kutosha katika maeneo yote ya mipaka.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.