Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Chifupa atolewa bungeni
Chifupa atolewa bungeni
By Habari Tanzania | Published  06/23/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, jana alimtoa nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), kutokana na kukiuka kanuni ya Bunge, kipengele cha mavazi.

Sitta alimtoa Chifupa wakati kipindi cha maswali na majibu kikiendelea.

Kutolewa kwake kulitokana na ‘kuchongewa' na baadhi ya wabunge ambao Sitta hakuwataja, ambao walihoji uvaaji wa mwanasiasa huyo chipukizi.

Amina alivalia vazi zuri - suti, yenye asili ya nchi za Ulaya na Marekani, na kufunika kichwa kwa kofia iliyofanana kwa rangi na nguo. Rangi yake ilikuwa nyeusi.

Katika utetezi wa uamuzi wake, Sitta alisema mavazi ya aina hiyo, yalipaswa yawe na ‘glovu' mikononi, lakini Chifupa hakufanya hivyo.

Baada ya amri hiyo, Chifupa alitoa nje, akavua kofia, kisha akarejea ukumbini akionekana amenyong'onyea.

Baadhi ya wabunge walimtetea kwa kumpelekea Spika taarifa za maandishi, ndipo kiongozi huyo aliposema kilichokosewa na Chifupa, ni kutovaa glovu zinazoendana na vazi hilo .

Nje ya ukumbi wa Bunge kulikuwa na mjadala miongoni mwa wabunge.

Wapo waliosema kuwa Chifupa hakupaswa kutolewa nje, kwani alivaa vizuri.

Kanuni iliyotumika kumtoa nje Chifupa ni ya 119(3) (iii). Kanuni hiyo inasomeka: “…Suti ya kiulaya ya kike, ama ikiwa kamilifu pamoja na kofia na ‘gloves' au bila vitu hivyo.”

Baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Koani, Haroub Said Masoud (CCM), aliomba mwongozo wa Spika.

Mbunge huyo alipendekeza ifanyike semina kwa wabunge kuhusu kanuni za Bunge kwani zaidi ya asilimia 50 ya wabunge wa sasa, ni wageni bungeni.

Spika alipokea mapendekezo hayo, na kusema Katibu wa Bunge ataandaa semina hiyo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.