Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Sumatra sasa yaamka
Sumatra sasa yaamka
By Habari Tanzania | Published  04/24/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
*Mabasi ya mikoani, daladala zote ukaguliwa leo
*Usafi wa sare za makondakta nao kuangaliwa

Na Mwandishi Wetu

MAELFU ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, huenda leo wakakumbwa na shida kubwa ya usafiri baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuamua kufanya operesheni maalum ya kukamata daladala zinazokiuka utaratibu.

Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray, ameliambia Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, kwamba maandalizi ya operesheni hiyo yamekamilika.

Mziray alisema operesheni hiyo maalum ya leo, itahusisha ukamataji wa makondakta na madereva wakorofi wa daladala, mabasi ya kubeba wanafunzi na mabasi ya mikoani yanayotoka au kuingia jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa daladala, operesheni hiyo itafanyika katika wilaya zote za jiji la Dar es Salaam na kwamba gari, madereva na makondakta watakaokamatwa, watapelekwa katika vituo vya polisi vitakavyopangwa.

Asilimia kubwa ya daladala zinazofanya kazi kati njia mbalimbali za jijini Dar es Salaam aidha zipo katika viwango visivyotakiwa au kuendesha huduma hiyo kwa abiria kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, hali ambayo inafanya kuwe na uwezekano mkubwa wa gari nyingi za aina hiyo kutokuwapo barabarani.

Tayari Sumatra imekwishawaarifu wamiliki wa daladala, mabasi ya mikoani na yale ya kubeba wanafunzi, wahakikishe madereva na makondakta wao wanafuata sheria za barabarani.

Mziray alisema miongoni mwa mambo yatakayohusika katika operesheni hiyo ni pamoja na ukaguzi wa leseni za usafirishaji kwa kuhakikisha daladala zinapita katika njia zilizopangwa na kupita barabarani na si pembeni.

Mziray alifafanua kwamba, kwa makusudi au kutofahamu, baadhi ya wasafirishaji wakiwemo wa mabasi yaendayo mikoani, huamua kutoa leseni ambazo ni za kughushi.

"Sumatra inawaagiza wasafirishaji  ambao hawana uhakika na uhalali wa leseni zao, walipaswa kufika katika ofisi za mamlaka kwa ajili ya kufanya uhakiki wa uhalali wa leseni zao kabla zoezi kuanza," alisema Mziray.

Mziray alisema operesheni hiyo ambayo itaendelea kuanzia leo, itahusisha pia ukaguzi wa ubora wa magari, huduma na utekelezaji wa masharti ya leseni.

Katika operesheni hiyo, kila msafirishaji atapaswa kuwa na leseni hai na halali ya usafirishaji katika basi lake, ratiba ya njia kwa mabasi ya kwenda mikoani na gari lipakwe rangi ya njia ambako leseni imeelekeza (kwa daladala).

Mziray aliongeza kuwa madereva na makondakta watapaswa kuvaa sare safi na zenye muhuri unaoonyesha namba ya gari wanayohudumia na kuhakikisha abiria wanapanda na kushuka katika vituo  vinavyostahili.

"Msafirishaji ambaye gari lake litakutwa na makosa yaliyotajwa hapo juu, atatozwa  faini hapo hapo kulingana na kosa lenyewe," alionya.

Alisema wasifirishaji ambao watakutwa na leseni za kughushi watatozwa faini kwa kosa la kufanya biashara ya usafirishaji  bila leseni na atashtakiwa mahakamani kwa kosa la kutumia leseni ya kughushi


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Didas Ngowi)
    Rating
    Dear Sumatra Team

    Kuna tabia imejitokeza kwenye vyombo vya usafiri (Daladala), Magari mengi sasa hivi yanakwenda Kivukoni ili abiria alipe nauli mara mbili ya kwenda na kurudi na Asubuhi hivyo hivyo kwa watu wengine sio tatizo lakini kwa wengi wetu ni matatizo makubwa kutokana na kipato chetu cha kila siku..



    DALADALA

    Ili kupunguza kero tunayoipta naomba yafautayo yafanyiwe kazi kutusaidia sisi tunaotumia usafiri wa Daladala kila siku
    Magari yote ya kivukoni yasajjliwe upya kupata uwiano wa Magari ya Posta na Kivukoni.
    Kama abiria amepanda Gari la Kivukoni na hashuki alipe nauli moja inayotambulika na Serikali (SUMATRA).
    Wale wote walio sajili Magari yao kinyemela kwa rout za Kivukoni wachukuliwe hatua za kindhamu kwa sababu kwao sasa hivi ni biashara hata zile Haice za Bugurini Posta nyingi zinakwenda Kivukoni kwa ajili ya hiyo 200/=.
    Katika utafiti nilioufanya baadhi ya abria nauli kwa sio tatizo tatizo ni pale unapozunguka na Gari bado usafiri unakuwa wa shida kwa sababu ya kukatiza rout, mfano Gari imetoka Mnazi mmoja Konda anasema ana kwenda Kivukoni anachukua 200 zake akifika Maeneo ya Peckoco anajifanya kuuliza kuna Abiria wa Kivukoni hakuna anakatiza vichochoroni huyo katoka na 200 zake amekusanya tayari, Abiria hana tatizo anachotaa awahi lakini mtu kama Mimi sikubali na ndipo ugomvi unapoanza.
    Mimi kama Abiria ninasikitishwa sana na matatizo ninayoyaona ya usafiri hasa kwa watu wazima, Mama wenye watoto na Wanafunzi kwa Jumla. Pia utakuta Trafic Polisi yuko Barabarani lakini cha maana anachosaidia hakuna zaidi ya kusababisha usafiri kuwa mgumui. Kituo chochote cha basi akiwepo Askari traffic usafiri siku hiyo ni wa shida sana hilo nimeliona na abiria hulalamika na kusema hayasimami kwa sababu kuna Trafic.
    Naomba sehemu zote za Junctio (sehemu ambazo Gari inaweza kugeuza ikarudi ilikotoka akae Trafic kuepusha kukatiza rout sio vituoni na mafanikio mtayaona.


    BRAKE DOWN

    Kuna Magari haya yanaitwa Brake Down magari haya yamekuwa kero kwa Jiji la Dsm na yanasababisha sana foleni, wahusika wote wa kwenye hayo magari sura zao ni za ajabu kwanza wananjaa kali hawana ubinadamu kuna siku kama ningekuwa na silaha basi ningefungwa kwa sababu amekuja mtu na mgonjwa wako hai hai wahusika wakamchukua mgonjwa wao wakaingia naye ndani Hospitali sisi wengine tupo nje tunashangaa siku hiyo nilikuwa lunch ghafla wakaja Brake down haraka haraka wakalifunga gari (Tanganyika jake) ikabidi niingilie na kuuliza jamani hawa watu wamekuja na mgonjwa wakanitolea macho kibaka ananafuu wakachukua gari wakaondoka kwa sababu nilikosa support.
    Magari haya ya Break down yamekuwa kero kwa wakazi wa Dsm kutokana na unyama wanaofanyiwa wenye magari watu hawa hawana ubinadamu wapo mitaani wanazunguka na magari kwa ajili ya kutafuta riziki kutoka kwa mwenye nacho na asiye kuwa nacho.
    Kwa kweli ndugu zangu kama mlishawahi kukutana na hii hali mtakakubaliana na haya ninayoyasema.
    Naomba kama huu mradi ni wa serikali basi watafute biashara nyingine ya kuongeza pato sio kwa mtindo huu unaofanyika sasa hivi. Kumbuka kuwa mji huu una magari mengi parking hakuna unatatizo la haraka unapaki gari mara moja na sehemu ya kupita magari mengine umeacha wanakuja wenye break down wanalichukua ni dhambi kubwa na ndio maana wenye break down wote afya zao ni Mbaya kutokana na uharamia wanaoufanya na hauompendezeshi Mwenyezi Mungu.

    Naomba nipewe mamlaka ya kukamata magari na kuandika namba ya magari yanayovunja sheria za barabarani ili niyawakilishe kwenu na kufanyia kazi.

     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.