Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Bandari kumejaa wezi’
Bandari kumejaa wezi’
By Habari Tanzania | Published  06/22/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

MBUNGE wa Ilala, Mussa Azzan (Zungu), amesema wizi umekithiri katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mbunge huyo alisema hayo juzi jioni bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya serikali iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji, wiki iliyopita.

Alisema wizi ni moja ya sababu zilizoifanya Uganda isipitishe tena mizigo yake katika bandari hiyo.

Sababu nyingine alisema ni ucheleweshaji mizigo ambao alisema umekithiri, ikilinganishwa na bandari nyingine.

Zungu alizungumzia pia suala la wawekezaji kwenye sekta ya madini, na kuhoji sababu zinazowafanya wageni hao washindwe kujenga majengo ya kisasa katika maeneo ya madini au katika miji kama Dar es Salaam .

Alisema miji kama Johannesburg imejengwa kwa dhahabu, lakini hapa nchini, utajiri wa madini unapelekwa nje.

Zungu ambaye aligusia mambo mengi kwa haraka haraka, alitoa rai maalumu kwa serikali kuhakikisha Barabara ya Uhuru inajengwa ili kuondoa msongamano na aibu, hasa kwa wageni wa kitaifa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.