Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali iwe makini na ahadi zake
Serikali iwe makini na ahadi zake
By Habari Tanzania | Published  04/22/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

KAMA kuna jambo baya kwa watu waliostaarabika, ambalo mara nyingi hushusha heshima ya mtu bila kujali wadhifa wake, ahadi za uongo au zisizotekelezeka.

Jambo hili haliishii kwa waliostaarabika tu, bali hata kwa watoto wadogo, ambao kama mzazi wao akizoea kuwadanganya kuwatimizia mahitaji yao au ahadi nyingine yoyote, watoto hao hupungukiwa na upendo kwa mzazi wao.

Tunatoa kauli hii kwa makusudi kabisa tukimaanisha ahadi za serikali yetu, lakini kauli yetu hii ina nia njema ya kuwakumbusha viongozi wetu kuwa ahadi nyingi wanazotoa bila kuzitekeleza zina madhara yake tena makubwa.

Tangu Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani, viongozi wake wakuu wamekuwa hawaishi tambo na majigambo.

Lakini kikubwa zaidi, wamekuwa mabingwa wa kutoa ahadi nyingi nzuri, ambazo utekelezaji wake umekuwa sawa na sifuri.

Ahadi zilizotolewa ni nyingi. Tunaamini kabisa kuwa serikali inajua imeahidi nini na imetekelezaje ahadi zake hizo, hivyo hatuna nia ya kuzirudia hapa, lakini tunashawishika kuikumbusha kuhusu ahadi yake kwa wanafunzi wa elimu ya juu kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa elimu ya juu kutokana na umaskini wa wazazi wake.

Ahadi hii ilitolewa na kiongozi mkuu wa nchi, Rais Jakaya Kikwete, wakati akizungumza na wasomi wetu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee katika maadhimisho ya miaka 30 ya kuzaliwa kwa CCM.

Rais Kikwete alitoa ahadi hii Februari 5 na tangu alipoitoa miezi miwili imekwishakatika, lakini utekelezaji hauonekani, wasomi bado wanasota kutafuta asilimia 40 ya ada wanayopaswa kuchangia.

Tunatambua kuwa serikali ina mipango mingi, hivyo utekelezaji wa jambo hili unaweza kuchukua muda, hatuna tatizo na hilo kwa sababu huo ndio ukweli. Lakini kinachotutatiza ni ahadi iliyotolewa, tunajiuliza hii ahadi ilitolewa kimakosa au kwa sababu ya kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wasomi wetu.

Tunaamini kabisa kuwa serikali inao uwezo wa kutekeleza ahadi yake ya kuwalipia ada wanafunzi wa elimu ya juu kwa asilimia 100 bila uchumi wa nchi yetu kuyumba au kutetereka.

Imani yetu inatokana na taarifa za hivi karibuni kuwa kuna ubadhirifu wa kutisha katika matumuzi ya serikali unaofikia sh bilioni 900, lakini pamoja na ubadhirifu huo, bado mambo yanakwenda na serikali inaendelea kusonga mbele na mkakati wake wa kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanapatikana.

Tena imani yetu hiyo inatokana na jitihada za makusudi zilizofanywa na Rais Kikwete za kuhakikisha kuwa klabu maarufu ya mpira wa miguu ya Hispania ya Real Madrid inakuja nchini kufanya ziara ya siku chache huku ikitumia mabilioni ya shilingi.

Hapo ndipo tunapojiuliza, inashindikana nini kwa Rais Kikwete aliyefanikiwa kuwashawishi wafanyabiashara na wadau wengine wa soka pamoja na Watanzania kwa ujumla, kuchanga mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kuileta timu ya Real Madrid, lakini ishindikane kuwahamasisha Watanzania na kuwaomba wahisani wa nje kuchangia kwa ajili ya ada ya wanafunzi wa elimu ya juu?

Hatuna nia ya kuingilia mpangilio wa kazi na vipambele vya kushughulikia mambo alivyojiwekea Rais wetu, lakini tuna haki ya kushangazwa na vitendo vyake kama mkuu wa taifa letu.

Tuna haki ya kushauri na kukosoa inapobidi na kwa mantiki hiyo tunahoji, serikali inashindwa nini kutekeleza ahadi zake, na kwa nini suala la wanafunzi wa elimu ya juu halipewi kipaumbele kama masuala mengine likiwamo la soka?


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Godfrey /Juma Mwanza)
    Rating
    The CCM government is good in good words but completely poor in actions! What is important as per now is to call upon opposition political parties to unite and have one candidate for 2010 presidency as a solution to the fishy CCM government, which is very expert in cheating the wananchi.
    High education is key to development in any country. It is for us a very serious issue as we are now talking of FAST-TRRACKING of East Africa federation,because there is a very immenant danger that all the professional jobs scarsly available in our country are going to be taken by Kenyans, becuase Kenya has excess professionals(graduates). TZ has very few graduates compared to other East African countries.Logically, TZ needs to invest much on Higher learning so as to cope with other East Adeican countries, otherwise TZ is going to be exploited by her other member countries.
    That criminal act of chasing studies(especially girls)from the campus shows that the current CCM government is not for WANANCHI but for CCM itself.Some girls who were chased by the government from the campus have acquired HIV/AIDS after being involed in immoral sexual acts so as to get money for food and accomodation, therefore this CCM government is responsible for that KILLING!
    Also, the CCM government knows that it is absolutely impossible for poor TZs(walalahoi)to pay for 40%. Where is the logic to chase students because of 40% which every rational human being knows that it is impossible to be afforded by the majority of TZs?
    CCM MUST GO OUT OF POWER BY 2010! BECAUSE IT IS KILLING HIGHER LEARNING EDUCATION IN TZ! FULL OF "FIRE WORKS" WITH EMPTY PROMISES! CCM IS NOT IN POWER FOR NATIONAL INTERESTS!BUT FOR THE FEW BIG LOGS! IT IS FULL OF CORRUPTION! IT MUST GO OUT!WE ARE TYRED OF IT!
     
  • Comment #2 (Posted by Godfrey /Juma Mwanza)
    Rating
    The CCM govnmnt must go by 2010 election, because it is against Higher learning education.It is talking of FAST trracking of EA federation, all the professional jobs in the TZ are going to be taken by Kenyans, because Kenya has excess professionals(graduates). By supressing High education, CCM govnmnt is SELLING OUR COUNTRY! WE MUST VOTE IT OUT BY 2010! WE CALL UPON OPPOSITION POLITICAL PARTIES TO UNITE SO AS TO HAVE ONE PRESIDENTIAL CANDIDATE BY 2010.CCM IS FULL OF "FIRE WORKS POLITICS" BY GIVING MANY PROMISES TO THE WALALAHOI SO AS TO WIN ELECTION.THE TIMES OF CHEATING HAVE GONE, WE WANT "ACTIONS NOT WORDS".
    SOME GIRLS WHO WERE CHASED BY CCM FROM THE UNIVR CAMUS OF LATE HAVE BEEN INFECTED WITH HIV/AIDS. CCM GOVNMNT IS A "KILLER" IT MUST GO!
    ALL WANANCHI MUST UNITE THEMSELVES ALL OVER THE COUNTRY AND MAKE NATIONAL WIDE DEMONSTRATIONS TO REMOVE CCM FROM POWER.CCM IS FULL OF EGOISTIC INDIVIDUALS WHO ARE AFTER THEIR STOMACHS, NOT THE COMMON GOOD OF THE MWANANCHI!
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.