Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ajali ya Buffalo yawazindua polisi
Ajali ya Buffalo yawazindua polisi
By Habari Tanzania | Published  04/20/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Daniel Mjema, Moshi

AJALI ya basi la kampuni ya Buffalo na lori iliyoua watu 22 na kujeruhi  18, imewazindua polisi mkoani hapa ambapo sasa wameanza kutumia kifaa maalumu kubaini magari (mabasi) yaliyo kwenye mwendo.

Matumizi ya kifaa hicho maalumu  kinachoweza kugundua mwendo wa gari likiwa mbali, kilianza kutumika juzi baada ya kuletwa mkoani Kilimanjaro kutoka  Makao Makuu ya Jeshi hilo, Jijini Dar es Salaa.

Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko, alithibitisha jana kutumiwa kwa kifaa hicho na kusema kuwa kwa juzi pekee magari manne likiwemo basi la kampuni ya Meridian limenaswa.

Ng'hoboko alisema magari hayo yalipigwa faini ya papo kwa hapo na kwamba madereva watakaobainika kurudia kosa la mwendo  kasi watashitakiwa mahakamani na kunyang'anywa leseni zao za udereva.

Hatua hiyo imekuja sambamba na Jeshi hilo kuwataka  abiria wenye haraka na kushabikia mwendo kasi wa mabasi watumie usafiri wa ndege kama kweli wana haraka za kufika wanakokwenda.

Kauli hiyo ilitolewa juzi  na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP), James Kombe, baada ya kukutana kwa faragha na polisi wa usalama barabarani mkoa wa  Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, bosi huyo wa Trafiki aliwataka abiria wenye haraka kusafiri siku moja kabla badala ya kusafiri siku hiyo hiyo na kutaka dereva aendeshe basi kwa mwendo kasi.

“kuna dhana ya kijinga sana unakuta abiria mmoja au wawili wanalalamikia mwendo kasi halafu wanatokea abiria wengine wanamkemea na kusema wana haraka…! Kama una haraka si upande ndege?” alisema na kuhoji Kombe.

Pia aliwataka abiria kuheshimu utaratibu wa kutopanda basi lililojaa maarufu na kusisitiza kwamba wakiona basi limejaa wapande basi lingine.

SACP Kombe alifafanua kuwa kikosi cha usalama barabarani kitaongezewa nguvu ili kukabiliana na madereva wakorofi wanaoendesha mabasi kwa mwendo kasi bila kujali maisha ya  abiria wa mabasi hayo.

Naye  Ally Sonda  anaripoti kuwa; maiti mwingine wa ajali ya basi hilo,Leonard Christian Saria(48) atambuliwa juzi jioni hivyo kufanya jumla ya miili ya marehemu iliyotambuliwa kufikia 20 sasa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema Saria alikuwa mkazi wa Msaranga Katika Manisapaa ya Moshi na kwamba alikuwa dereva.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo maiti  ambazo hadi jana jioni zilikuwa hazijatambuliwa na ndugu au jamaa zao ni mbili ikiwemo ya Mwanamke na Mwanume, wote watu wazima.

Kamanda Nghoboko amewataka wananchi kuendelea kufika kwenye chumba cha maiti Hospitali ya Mawenzi kuitambua miili hiyo.

Alisema hali za majeruhi wa ajali hiyo, akiwemo dereva wa basi la Bufallo zinaendelea vizuri kwenye Hospitali za Mawenzi  na KCMC ambako wamelazwa kwa matibabu.

Na Omary Magongo, anaripoti toka Arusha, kuwa Chuo Kikuu cha Arusha (UoA) ni miongoni mwa
taasisi ziliathiriwa na tukio hilo baada ya mwanafunzi wao mmoja kufariki dunia katika ajali hiyo.

Akitoa taarifa rasmi ya kifo hicho kwa wanafunzi jana, Mkuu wa Kitivo  cha Biashara na Uhasibu chuoni hapo, Cosmas Nyarusanda, alimtaja mwanafunzi
huyo kuwa ni Benedict Maufa aliyekuwa mwaka wa pili katika kitivo hicho.

Nyarusanda alisema mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma masomo ya jioni katika tawi la chuo hicho la Arusha mjini, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na mipango ya kuusafirisha kwenda kwao Ukerewe kwa mazishi inafanywa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.