Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Warioba kuongoza timu ya Madola uchaguzi Nigeria
Warioba kuongoza timu ya Madola uchaguzi Nigeria
By Habari Tanzania | Published  04/11/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu


WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Don McKinnon, kuongoza timu maalumu ya waangalizi wa jumuiya hiyo, katika uchaguzi mkuu wa Nigeria.

Uchaguzi wa rais na bunge wa Nigeria, unatarajiwa kufanyika Aprili 21, mwaka huu.

Hii si mara ya kwanza kwa Jaji Warioba kuongoza timu ya waangalizi wa Jumuiya ya Madola katika chaguzi. Aliwahi kuongoza timu kama hiyo katika uchaguzi mkuu wa Malawi.

Aidha, ameshashiriki katika timu zilizoangalia chaguzi katika nchi za Zambia, Nigeria na Ethiopia.

McKinnon alisema timu hiyo inapelekwa kufuatia ombi lililotolewa na Serikali ya Nigeria na Tume Huru ya Uchaguzi ya nchi hiyo.

Alisema timu hiyo itakuwa na wajumbe tisa ambao ni watu maarufu, watakaosaidiwa na wajumbe saba wa sekretarieti ya jumuiya hiyo.

Pamoja na Jaji Warioba, wajumbe wa timu hiyo ni Joseph Biribonwa, ambaye ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda, Omar Jallow, Kaimu Katibu Mkuu na kiongozi wa Chama cha People’s Progressive cha Gambia na Dk. Noor Mohammad, Naibu Kamishna wa zamani wa Tume ya Uchaguzi ya India.

Pia wamo Robert Patterson, Afisa wa Uchaguzi wa zamani wa Columbia, Kareen Payne, mwakilishi wa kundi la vijana toka Antigua na Barbuda, Sheila Roseau naye kutoka Antigua na Barbuda, Nancy Tembo, mbunge toka Malawi na Martin Tete, Ofisa Mwandamizi wa uchaguzi kutoka Vanuatu


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.