Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  100 wazaliwa Dar mkesha wa Pasaka
100 wazaliwa Dar mkesha wa Pasaka
By Habari Tanzania | Published  04/9/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
 Sheilla Sezzy

JUMLA ya watoto 100 wamezaliwa jijini Dar es Salaam katika mkesha wa Sikukuu ya Pasaka, iliyoadhimishwa jana duniani kote.

Kwa mujibu wa Ofisa Muuguzi wa Hospitali ya Temeke, Bahati Hamisi, jumla ya watoto 30 walizaliwa siku hiyo katika hospitali hiyo. Alisema kati yao, 15 ni wa kike na wa kiume ni 15 pia.

Ofisa huyo alisema kuwa watoto wote wamezaliwa salama na hali zao na za mama zao zinaendelea vizuri.

Katika Manispaa ya Ilala, jumla ya watoto 32 walizaliwa katika mkesha huo. Ofisa Muuguzi wa Hospitali ya Amana, Enjoy Kilangi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kati ya watoto hao, 23 ni wa kike na tisa ni wa kiume.

Aidha, alifafanua kuwa akina mama wawili walijifungua mapacha. Mama mmoja alijifungua mapacha wote wa kike wakati mama mwingine alijifungua mtoto wa kiume na wa kike.

Taarifa iliyotolewa na muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Mwananyamala, Grace Kombe, inaonyesha kuwa watoto 26 walizaliwa katika hospitali hiyo. Kati yao 13 ni wa kiume na 13 wengine walikuwa wa kike.

Katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili (MNH), jumla ya watoto 12 walizaliwa, kati ya hao, wa kike ni watano na wa kiume saba.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.