Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kipigo kisiikatishe tamaa Yanga
Kipigo kisiikatishe tamaa Yanga
By Habari Tanzania | Published  04/9/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

IJUMAA iliyopita, wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa, Yanga ya jijini Dar es Salaam, ilicheza mechi yake ya awali ya hatua ya tatu ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mechi hiyo iliyopigwa siku hiyo mjini Tunis, Tunisia, Yanga walifungwa 3-0, hivyo kulazimika kujipanga vema kwa mechi ya marudiano itakayochezwa nchini.

Ni wazi, kipigo hicho, kimeipa Yanga wakati mgumu kwani ili iweze kuvuka kikwazo, italazimika kushinda mabao 4-0, kitu ambacho si kazi ndogo.

Tunasema si kazi ya ndogo kutokana na uzoefu wa Esperance katika michuano ya kimataifa, kwani kwa ushindi wake wa mechi ya awali, inaweza kutumia dakika 90 kujihami tu.

Ingawa kipigo hiki kinaonekana ni kikubwa, lakini mchezo wa soka ni makosa, hivyo kama Yanga watapanga vema karata zao, si kitu cha miujiza kuvuka kikwazo.

Kipigo cha Tunis, kinapaswa kushughulikiwa kwa umakini zaidi, kwani ikicheza nyumbani, Yanga pia inaweza kupata ushindi mnono wa kutosha kuivusha hatua inayofuata.

Yanga wakiwa wenyeji wa mechi ijayo, wanalazimika kuchukulia kipigo cha Tunis kama changamoto ya kujipanga zaidi kwa mechi ya marudiano badala ya kuanza kunyoosheana vidole.

Mifano ni mingi ya kueleza ni kwa jinsi gani timu inaweza kufungwa mabao mengi ugenini, lakini ikajipanga vema na kushinda kwa idadi kubwa zaidi, hivyo kusonga mbele.

Kazi kubwa ambayo makocha na viongozi wanatakiwa kuifanya ni kuwarejesha wachezaji kwenye hali ya kawaida, kwamba wanaweza kushinda na kuvuka kikwazo.

Ingawa, inahitaji mikakati kabambe, lakini wachezaji wa Yanga, wanapaswa kujiuliza kama, Esperance waliweza kushinda mabao 3-0 nyumbani, kwanini wao washindwe kuupiku ushindi huo CCM, Kirumba, Mwanza.

Tunayasema haya, kwa kutambua kuwa penye nia pana njia, hivyo kama Wanayanga watashikamana katika kuiandaa timu yao kimazoezi na kisaikolojia, Yanga bado inaweza kuvuka.

Tunasema ni kuvuka kwa sababu, suala hapa Yanga si kushinda, bali inapata ushindi wa kiwango gani, kwani ili iweze kuvuka, inahitaji kushinda 4-0.

Rekodi zinaonyesha kuwa, ingawa inaweza kuonekana ni kitu kigumu, lakini katika soka, inawezekana kwani kama timu ilifungwa ugenini, nayo inaweza kushinda mechi ya nyumbani.

Kutokana na hayo, shime kwa wachezaji, makocha, viongozi na wanachama wa Yanga kujipanga upya katika kuhakikisha timu yao inashinda katika mechi ya marudiano.

Ingawa Yanga italazimika kucheza kwa tahadhari kutokana na mazingira yaliyojitokeza kwenye mechi ya Aprili 6, tunaamini uwezo wa kuifunga Esperance na kuvuka kikwazo, ungalipo.

Kitu cha msingi, ni kuwajenga wachezaji wote wakiwamo wale wenye kadi za njano kwamba, siku hiyo wasifanye makosa, kwa kuepuka hatari ya kulimwa kadi ya pili, hivyo kwenda nje.

Suala la mchezaji Hamis Yusuf kulimwa kadi nyekundu, Said Maulid ‘SMG’, kuumizwa, huku wengine watano wakipewa kadi za njano, ni wazi, kulichangia kipigo cha Tunis.

Kama wachezaji, kocha mkuu, Mserbia, Sredojevic Milutin ‘Micho’, wachezaji na viongozi wataondoa hali ya kukata tamaa, kwenye mechi ya marudiano, lolote laweza kutokea.

Tunayasema haya, kwa kuzingatia kuwa, hakuna kitu kibaya kama kukata tamaa, kwani kama hivyo ndivyo, kulikuwa hakuna haja ya Yanga kuingia mashindanoni.

Muhimu ni kwamba, Yanga ingali na nafasi ya kupata ushindi mzuri wa kuivusha katika hatua ya nne, ambayo ina manufaa makubwa kwa timu husika.

Kama wadau wa maendeleo kwa ujumla, shime wanachama wa Yanga, huu ndio wakati muafaka kwa wao kujipanga upya kwa ajili ya kutafuta ushindi mnono katika mechi ya marudiano.

Ni wazi, licha ya kufungwa katika mechi iliyopita, makocha na wachezaji wa timu zote, watakuwa wamesomana, hivyo Micho, anapaswa kutumia udhaifu wa Esperance kulipa kisasi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.