Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  CCM kumtimua diwani wake anayetuhumiwa kubaka
CCM kumtimua diwani wake anayetuhumiwa kubaka
By Habari Tanzania | Published  04/6/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Moses Mabula, Uyui


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, mkoani Tabora, kimepanga kumvua madaraka, Diwani wa Kata ya Ndono, Musa Kayege, ambaye hivi karibuni alifikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14.

Habari kutoka ndani ya CCM wilayani hapa, zinasema kuwa mipango ya kumvua diwani huyo madaraka, imeshaandaliwa. Habari hizo zimeongeza kuwa, kwa kulinda heshima ya chama hicho, diwani huyo atatakiwa kutangaza kujiuzulu.

Inaelezwa kwamba tuhuma zinazomkabili diwani huyo zimekishushia hadhi chama hicho.

Baadhi ya madiwani waliozungumza na gazeti hili lakini wakakataa majina yao kutajwa, walisema kuwa kitendo hicho kimewafedhehesha hata wao.

Walisema kuwa hivi sasa kila wanapopita mitaani wamekuwa wakizomewa huku wakiitwa madiwani wabakaji.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hamisi Bundala alisema tuhuma zinazomkabili diwani huyo ni nzito na zinawatia doa.

Alisema tangu mwenzao huyo afikishwe mahakamani, wamekuwa na wakati mgumu kwani baadhi ya viongozi wa kambi ya upinzani wamekuwa wakiwakejeli.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui, Abdallah Kazwika, hakuwa na jibu la moja kwa moja kuhusu hatima ya diwani huyo mwenye tuhuma za ubakaji.

Alisema kwa sasa hawezi kusema chochote kwa kuwa suala hilo bado lipo katika vyombo vya sheria, lakini iwapo atatiwa hatiani, atafukuzwa uongozi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by kasigala)
    Rating
    Aksante sana kwa vyombo vya habari kwa kuanika maovu yanayotendeka na baadhi ya viongozi wa Nchi hii Tanzania kwani ni mara ngapi?VIONGOZI wetu hawa tuliowachagua wenyewe wanageuka kuwa mamba? ni mara ngapi tumepata kusikia matukio kama haya yakusikitisha tena viongozi wetu wenyewe,Kwani ninanukuu kiogozi mmoja wilayani singida mme mheshimiwa katika serikari yetu ambaye alimpa mimba mwanafuzi' Viongozi wetu mnatupeleka shimoni kwani RAIA wema tukimbilie wapi? Maoni yangu kwa SERIKALI IWE CHINI YA MAHAKAMA NA SI MAHAKAMA IWE CHINI YA SERIKALI ILI KIONGOZI WA SERIKALI AWEZE KUHUKUMIWA APATIKANAPO NA HATIA KAMA RAIA WENGINE.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.