Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Hakuna visa kuingia Afrika Kusini
Hakuna visa kuingia Afrika Kusini
By Habari Tanzania | Published  04/6/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Tamali Vullu


SERIKALI ya Tanzania na Afrika Kusini, zimesaini mkataba wa kufuta matumizi ya viza za kusafiria kati ya nchi hizo.

Kusainiwa kwa mkataba huo, pamoja na mingine kadhaa, ni matokeo ya mazungumzo yaliyohusisha timu zilizoongozwa na Rais Jakaya Kikwete (Tanzania) na Thabo Mbeki (Afrika Kusini).

Makubaliano hayo yalitiwa saini jana kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Joseph Mungai na wa Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Ngaqula.

Rais Kikwete na Mbeki walishuhudia utiaji saini huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam.

Akizumgumza na waandishi wa habari, Kikwete alisema kwa kuanzia, matumizi ya viza kwa watu wanaosafiri baina ya nchi hizo mbili, yataondolewa kwa maofisa wa serikali.
Hata hivyo, hakueleza itachukua muda gani kwa raia wa kawaida kuruhusiwa kusafiri bila viza wanaposafiri katika nchi hizo.

Pia Waziri Mungai na Mapisa-Ngaqula wa Afrika Kusini, walisaini mkataba wa uhamiaji ambao nchi hizo zitaangalia ni namna gani watashughulikia masuala yao.

Mkataba mwingine uliosainiwa jana ni wa ushirikiano katika masuala ya bahari ambao utahusu utoaji wa mafunzo na masuala ya uokoaji kati ya nchi hizo mbili. Ulisainiwa na Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge na Waziri wa Usafirishaji wa Afrika Kusini, Jeff Rabede.

Awali, akifungua mkutano wa kamisheni ya uchumi ya raia kati ya Tanzania na Afrika Kusini, Rais Kikwete alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini ni wa muda mrefu na kwamba kuundwa kwa Kamisheni ya Uchumi ya Rais (Presidental Ecomonic Commission) ni njia mojawapo ya kuimarisha ushirikiano huo, hasa katika masuala ya uchumi. Kamisheni hiyo iliundwa Septemba 2005.

“Uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili, unaleta matumaini. Hata hivyo, tunapaswa kuendelea mbele zaidi na katika mkutano huu tutajadili kipi hasa kinahitajika kufanyiwa kazi ili tusonge mbele.

“Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, kiwango cha biashara kati ya nchi zetu mbili, kimeongezeka kutoka dola milioni 314.9 hadi dola milioni 696.3 kati ya mwaka 2003 na 2005,” alisema Rais Kikwete.

Alisema usafirishaji wa bidhaa za Tanzania kwenda Afrika Kusini umeongezeka kutoka dola milioni 38 mwaka 2003 hadi dola milioni 292 mwaka 2005 na kwamba uingizaji wa bidhaa kutoka Afrika Kusini umeongezeka kutoka dola milioni 277 hadi dola milioni 404 katika kipindi hicho.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha kuwa, Afrika Kusini ni kielelezo cha ufanisi wa ushirikiano wa kibiashara na Tanzania, hata hivyo hakuna uwiano katika biashara, lakini hilo linaweza kurekebishwa kwa Tanzania.

Afrika Kusini ina mahitaji makubwa ya soko kutoka Tanzania kuliko ilivyo Tanzania kwa Afrika Kusini.

“Afrika Kusini ni nchi ya tano kwa ukubwa kuwekeza Tanzania baada ya Uingereza, Kenya, India na China. Takwimu zinaonyesha kuwa, kati ya mwaka 1990 na 2006 uwekezaji kutoka Afrika Kusini umeongezeka hadi kufikia dola milioni 467, hiyo ni sawa na asilimia 10 ya uwekezaji wote nchini Tanzania katika kipindi hicho,” alisema Kikwete.

Alisema zaidi ya kampuni 150 kutoka Afrika Kusini zinafanya shughuli zake Tanzania, mojawapo ya hayo ni Anglo-Ashanti Gold inayojihusisha na masuala ya madini na AFGEM, Ilovo Group ambao wanamiliki kiwanda cha sukari Kilombero.

Hata hivyo, alisema Tanzania bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika masuala ya miundombinu, nishati, teknolojia ya mawasiliano na akasema serikali inafanya iwezalo kurekebisha vikwazo katika masuala hayo.

Naye, Rais Mbeki alisema nchi yake itashirikiana na Tanzania katika kuondoa vikwazo hivyo, ili masuala hayo yaweze kwenda vizuri


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.