Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Majambazi wampiga risasi polisi
Majambazi wampiga risasi polisi
By Habari Tanzania | Published  03/30/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Anna Makange, Lushoto


ASKARI wa Jeshi la Polisi wilayani Korogwe mwenye namba F. 5002, D/C Mohamed, amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi sehemu za tumboni na mapajani katika harakati za kumkamata mmoja wa majambazi waliokuwa wameliteka basi la Kwekanga Line, lililokuwa likitokea wilayani Lushoto kuelekea jijini Tanga.

Majeruhi huyo amelazwa katika hospitali ya serikali Magunga, Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Issaya Mngulu, ambaye alikuwa mmoja wa wapiganaji katika tafrani ya kurushiana risasi baina ya polisi na majambazi hao, alisema askari huyo alipigwa risasi na mmoja wa majambazi ambaye alikuwa akitumia bunduki aina ya gobori.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 11:00 alfajiri katika eneo la Mandui Mlola, Wilaya ya Lushoto, baada ya kundi la majambazi kuvamia basi hilo lenye namba za usajili T165 ADD, aina ya Fuso, lililokuwa likiendeshwa na Nassoro Ramadhani (31).

Mngulu alisema majambazi hayo yapatayo 10, yaliweka magogo barabani ili kuzuia gari hilo lisiweze kupita, na basi hilo liliposimama walilivamia na walifanikiwa kuwanyang’anya abiria waliokuwa zaidi ya 15 pamoja na dereva simu tano za mkononi zenye thamani ya sh 330,000 na vitu vingine vyenye thamani ya sh milioni 2.633.

Alisema katika msako aliouongoza yeye mwenyewe kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya za Lushoto na Korogwe, walipambana na majambazi matano juzi majira ya saa 5:00 usiku.

Alisema katika mapambano hayo, walirushiana risasi na hivyo kufanikiwa kumkamata Omar Said (40), katika eneo la Mlingano wilayani Korogwe.

Aidha, alisema kutokana na upekuzi walioufanya nyumbani kwa mtu huyo aliyekamatwa, katika eneo la Makorora walikamata pia simu za selula tatu, fedha taslimu sh 213,000, pamoja na mifuko ya sulphate mitano iliyotobolewa kwa ajili ya kuficha sura.

Mngulu alisema imebainika kwamba mwenyeji mshiriki kwenye tukio hilo ni Said Athumani, maarufu kwa jina la Side, mkazi wa Mlola, wilayani Lushoto, ambaye inadaiwa kuwa aliwahi kufungwa kifungo cha nje baada ya kupatikana na hatia ya kosa la wizi, ambapo kufuatia tukio hilo la Machi 28 alitoroka kijijini kwake.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.