Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  IGP Mwema amwondoa Mkuu wa Trafiki
IGP Mwema amwondoa Mkuu wa Trafiki
By Habari Tanzania | Published  03/29/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Agnes Yamo


MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, amefanya mabadiliko ya ghafla katika vitengo viwili ndani ya jeshi hilo, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuongeza ufanisi.

Habari zilizoifikia Tanzania Daima kutoka makao makuu ya jeshi hilo, zinaeleza kuwa IGP Mwema amefikia uamuzi huo ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika vitengo hivyo.

Moja ya vitengo vilivyokumbwa na mabadiliko hayo ni Kikosi cha Usalama Barabarani, ambapo Mkuu wa Kikosi hicho nchini, Mselemu Mtulia, ameondolewa katika nafasi hiyo.

Taarifa zilizopatikana zinaonyesha kuwa Mselemu amehamishiwa makao makuu ya jeshi hilo. Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja atapewa kazi gani.

Habari hizo zilieleza kuwa nafasi yake itachuliwa na James Kombe, ambaye kabla ya mabadiliko hayo alikuwa Mkuu wa Kikosi cha askari wa Kutuliza Ghasia (FFU).

“Sheria inampa mamlaka IGP kufanya mabadiliko wakati wowote anapoona kuna mahitaji au ulazima wa kufanya hivyo akijiridhisha. Kwa mfano, akiona malengo yanayotarajiwa hayakufikiwa,” alisema mmoja wa wapasha habari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ambaye hakupenda jina lake litajwe.

Alipotakiwa abainishe ni kwa nini mabadiliko hayo yamevigusa vitengo hivyo wiwili tu, alikataa kuingia kwa undani lakini alisema kuwa mtu anapewa kitengo kulingana na utendaji wake, lakini pia kuna vigezo vingine vingi vya kipolisi ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya wakubwa.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani anayehamishwa, Mselemu Mtulia, alikiri kuwapo kwa mabadiliko hayo.

“Ni kweli mabadiliko hayo yametokea, lakini ni ya kawaida kabisa, na tumeshakabidhiwa barua wiki moja iliyopita na leo (jana) ndiyo ninakwenda kuripoti makao makuu, lakini suala la makabidhiano ya ofisi za awali ni kesho,” alisema Kamanda Mtulia.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.