Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JWTZ kuwakabili Wasomali Longido
JWTZ kuwakabili Wasomali Longido
By Habari Tanzania | Published  03/22/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Ramadhani Siwayombe

RAIS Jakaya Kikwete amewaondoa hofu wakazi wa Wilaya ya Longido kuhusu uvamizi wa mara kwa mara unaofanywa na watu wanaoaminika kuwa majangili kutoka Somalia, na kusema kuwa iwapo Jeshi la Polisi litashindwa kukabiliana nao, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TJTZ), litapewa jukumu hilo.

Akihutubia mkutano wa hadhara mjini hapa juzi, Rais Kikwete alisema kuwa serikali tayari imeshaimarisha ulinzi na kwamba hatua zaidi zitachuliwa iwapo majangili hao wataendelea na uvamizi wao.

Aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari ya Samunge na kuzindua jengo la ofisi mpya ya Kijiji cha Malloni wilayani hapa.

“Hatutavumilia kuona nchi yetu inachezewa na wahuni wachache wakiwafanya wananchi kuishi kwa woga, wala kuichezea nchi… tutahakikisha tunawashughulikia na kama Jeshi la Polisi litashindwa, Jeshi la Wananchi litafanya kazi hiyo,” alisema Kikwete.

Alisema kuwa baada ya kuona msako dhidi yao umeimarishwa, Wasomali waliowavamia watalii mapema mwezi uliopita, wametokomea nchi jirani ya Kenya na hivyo kuwataka wananchi kuondoa hofu.

Wakati huo huo, Rais Kikwete alisema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mpango wa kujenga barabara ya Mugumu hadi Monduli kwa kiwango cha lami, ambayo haitapita katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Alisema barabara hiyo pia itainufaisha Wilaya ya Longido na kupunguza tatizo la ubovu wa barabara linaloikabili wilaya hiyo. Alisema barabara hiyo itapita katika Wilaya ya Longido katika vijiji vya Ngarasero hadi katika mji mdogo wa Mto wa Mbu.

Katika jitihada za kuboresha maendeleo katika wilaya hiyo, aliwataka wananchi kuhakiksha wanachukua hatua kukipandisha hadhi Kituo cha Afya Loliondo kuwa na hadhi ya hospitali.

Akizungumzia elimu, aliwaeleza viongozi na wananchi katika mkutano huo kuwa hajaridhika na kiwango cha wanafunzi waliofaulu kujiunga na elimu ya sekondari mwaka huu, kwani takwimu zinaonyesha kuwa wilaya hiyo ndiyo ya mwisho kwa kufaulisha.

Awali, katika taarifa ya mkoa, ilielezwa kuwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka jana walifaulu kwa asilimia 73 na nusu yao walichaguliwa kujiunga na sekondari katika awamu ya kwanza na waliobaki wote wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya shule zilizokuwa zinajengwa kukamilika.

Rais Kikwete yupo katika ziara ya mkoa wa Arusha ambapo pamoja na kukagua shughuli za maendeleo, pia anatumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu uliomuweka madarakani.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.