Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »   Wamuomba rais aruhusu wanyongwe
Wamuomba rais aruhusu wanyongwe
By Habari Tanzania | Published  03/20/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Asha Bani

KATIKA kile kinachoonyesha kuwa maisha ya wafungwa gerezani ni mabaya sana, wafungwa wawili wamemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, wakimuomba abatilishe adhabu ya kifungo cha maisha wanayotumikia ili wanyongwe hadi kufa.

Katika waraka huo ambao Tanzania Daima imepata nakala yake, wafungwa hao wanadai kuwa, kifo ni bora kulinganisha na tabu na mateso wanayoyapata wakiwa wafungwa wa maisha.

Katika barua hiyo, wafungwa hao kutoka gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam (majina na namba zao tunazihifadhi), wanamuomba Rais Kikwete atoe amri ya wao kunyongwa ili waepukane na mateso wanayoyapata hivi sasa.

Nakala ya barua hiyo iliyopitishiwa kwa Kamishna Mkuu wa Magereza, imetumwa pia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mkuu wa Magereza Mkoa (RPO).

Mmoja wa wafungwa hao anaeleza katika barua hiyo kuwa, alikamatwa mwaka 1977 kwa kosa la mauaji na kuhukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1983.

Hata hivyo, alisema kuwa mwaka 2002 alipata msamaha wa rais na adhabu yake ikapunguzwa na kuwa ya kifungo cha maisha.

Mfungwa mwingine, anadai katika barua hiyo kuwa, alikamatwa mwaka 1984 na kuhukumiwa adhabu ya kifo Februari 15, 1989.

Anasema kuwa, mnamo Mei 15, 2005 alipata msamaha wa rais na adhabu yake ikapunguzwa na kuwa kifungo cha maisha.

Katika barua yao, wanasema tangu wabadilishiwe adhabu hiyo, maisha yao yamekuwa ya tabu na shida kubwa kutokana na mateso wanayokumbana nayo gerezani na sasa wanatamani afadhali wangenyongwa.

“Kutokana na maisha ya gerezani kuwa magumu na ya tabu sana, tumefikia uamuzi wa hiari, Mheshimiwa Rais tunaomba utubadilishie uamuzi wako wa msamaha wa kifungo cha maisha na tuhukumu tena kunyongwa kwa kuwa tumechoka na tabu za huku gerezani Ukonga,” wanasema wafungwa hao katika barua yao.

Hivi karibuni, mahabusu katika gereza la segerea nao walizungumzia maisha magumu wanayoishi gerezani humo.

Waliyasema hayo kufuatia mgomo wa siku nne wa mahabusu kugoma kusikiliza kesi zao mahakamani, uliowalazimisha mawaziri wanne kutembelea gereza la Keko na kuzungumza na mahabusu hao.

Mgomo wao ulichochewa na kuachiwa haraka kwa dhamana kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, anayekabiliwa na mashitaka ya mauaji bila kukusudia.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.