Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Gharama haziepukiki katika demokrasia
Gharama haziepukiki katika demokrasia
By Habari Tanzania | Published  03/19/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Yahya Charahani

UCHAGUZI katika mazingira yoyote yale unatarajiwa kuwa alama na/au ishara ya demokrasia.

Unatarajiwa pia kuwa kioo cha mafanikio ya ushiriki wa wananchi katika masuala mbalimbali yanayohusu maisha yao.

Unatarajiwa kuwatoa katika hali mbovu kwenda katika hali bora, iwe kimaamuzi, kimaisha, kiuchumi, ukiacha chaguzi zile zinazoendeshwa kama kiini macho.

Lakini hapa kwetu Tanzania, uchaguzi umekuwa ishara ya watu wachache kuneemeka, wengine kuteswa, kudhalilishwa, kurubuniwa, kunyimwa kupiga kura, vitisho, wizi wa kura, kupata maumivu na wakati mwingine kupoteza viungo.

Zipo aina nyingi za uchaguzi, lakini tunapozungumzia uchaguzi wenye manufaa ni ule unaoheshimu demokrasia na matakwa ya raia wake walio wengi.

Baba wa demokrasia na baba wa taifa la Marekani, Thomas Jefferson alipata kusema kuwa demokrasia ina gharama kubwa na hazikwepeki katu na kwamba ni za milele.

Ukichunguza kwa undani kauli hii utagundua kuwa hakuna u-cheap katika demokrasia, inabidi wahusika kuingia gharama ili kuweza kukidhi matakwa ya walengwa.

Ikumbukwe kwamba walioifikisha demokrasia hapa tulipo waliingia gharama kubwa na wengine ikawagharimu maisha yao.

Kwa kawaida demokrasia haijileti yenyewe na katu haitarajiwi kujileta na ndiyo maana hapo suala la gharama linapoingia.

Demokrasia ni ya watu na watu ndiyo wanaotakiwa kujiamulia mustakabali wao katika wakati husika.

Demokrasia bora siyo ya watu wachache kuwachagulia wengi mtu wanayemtaka, inahitaji ushiriki wa wengi ili kuweza kukamilika.

Juzi Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali mbali ombi la Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, la kusitisha uchaguzi mdogo wa Tunduru na kuruhusu uchaguzi huo ufanyike kesho kama ilivyopangwa.

Na Kabla ya hapo Tume ya Uchaguzi ilipata kuzungumzia suala hili na ikalifafanua kwa upande wake, lakini bado tatizo likawa limeachwa bila kuwa na suluhisho.

Sina shaka na hoja za waheshimiwa hawa kutoa maamuzi yao, lakini napata shaka kama kweli tumekuwa makini kuitetea demokrasia.

Kimantiki ni ngumu kuweza kuridhisha kila upande, lakini kiuhalisia inapaswa wengi wapewe ili kusudi waweze kujiamulia mustakabali wao wenyewe.

Hivi kama hawa wananchi zaidi ya 11,000 wanakosa haki ya kupiga kura leo thamani ya yao kama watu itawekwa wapi?

Mbona thamani hii haikuonekana mwaka juzi ulipoahirishwa uchaguzi wa rais baada ya kufariki aliyekuwa mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya Chadema, Jumbe Rajab Jumbe.

Kwani ina maana demokrasia ina gharama katika ngazi za chini tu na za juu haina gharama katika ngazi za chini au kuna maana gani zaidi?

Kama tuko tunahitaji kujenga heshima na misingi ya demokrasia basi inatubidi tuingia gharama kubwa ili kuweza kuweka misingi kwa vizazi vijavyo.

Na misingi hii inapaswa kuanzia kuijenga demokrasia kuanzia katika ngazi za chini kabisa ili kusudi ngazi za juu ziwe imara.

Kama wanavyosema wanazuoni kila kizazi na malengo yake na aina yake ya maisha, basi sisi tuchague kuweka misingi bora kwa ajili ya demokrasia yetu.

Kiasi cha Sh. milioni 250 au bilioni 1.7 zilizotumika na vyama katika kampeni na michakato mingine kama hiyo hazipaswi kuwanyima haki watu wetu kupiga kura.

Hazifai pia kuwafanya watu wetu huko Tunduru wachaguliwe mbunge na watu wengine wachache ambao huenda wakawa wameandaliwa kwa ajili ya kukipendelea chama fulani.

Wananchi wetu wanahitaji kuwa na chaguo na kuwa na maamuzi na si kuamuliwa na watu wengine ili kusudi hao wengine waongoze maisha yao.

*Yahya Charahani ni Kaimu Mhariri wa Mwananchi Jumapili.
Anapatikana kwa email:charahani@yahoo.com Gazeti Tando: charaz.blogspot.com


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.