Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Uchaguzi Tunduru shwari, matokeo yaanza kutolewa
Uchaguzi Tunduru shwari, matokeo yaanza kutolewa
By Habari Tanzania | Published  03/19/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Muhibu Said, Tunduru

UCHAGUZI mdogo wa Jimbo la Tunduru, ulifanyika kwa amani jana, lakini kukiwa na malalamiko baadhi ya watu kuzuiwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 1.00 asubuhi, na katika baadhi ya maeneo, idadi ya watu waliojitokeza ilikuwa chache.

Uchache wa wapiga ura waliojitokeza unadaiwa ulisababishwa na baadhi ya watu waliojiandikisha kupoteza kadi zao za kupigia kura.

Wapiga kura tisa walizuiwa katika kituo cha Muungano mjini hapa, baada ya picha zao zilizozopo kwenye kadi za kupigia kura kuwa zimefifia na wengine kukosa kumbukumu zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Baadhi ya wapigakura ambao wana kadi lakini kumbukumbu zao hazionekani kwenye daftari la kudumu ni Ally Said (75) mwenye kadi namba 03780464, Ismail Chande (34) kwenye kadi namba 03780208 na Rashid Yusuf (33) ambaye alikuwa na kadi namba 40454420.

Wapigakura hao walisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, waliruhusiwa kupiga kura kwa dharura na kwamba kilichowashangaza ni kuwa hadi sasa tatizo lao halijatatuliwa.

Baadhi ya viongozi wa CUF, waliongozwa na Mkurugenzi wa Kikundi chao cha ulinzi cha Blue Guard, Said Miraji, jana asubuhi walikuwa wanahaha kutafuta ufumbuzi wa suala la watu hao kuzuiwa kupiga kura.

Pamoja na tatizo hilo, kwa ujumla hali ilikuwa ya utulivu. Mgombea kupitia chama DP, Richard Mayaya, alilieleza Mwananchi kuwa upigaji kura ulikuwa unaenda vizuri na alikuwa na matumaini ya kushinda uchaguzi huo.

Mgombea wa CCM, Mtutura Abdallah, ambaye alipiga kura katika Kijiji cha Ligoma saa 2.00 asubuhi, alisema ulinzi uliokuwepo ulitoa fursa kwa upigaji kura kwenda vizuri. Aliahidi kukubaliana na matokeo ya aina yoyote.

Kwa upande wake, Mgombea wa CUF, Mazee Rajab, aliyepiga kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Muungano mjini hapa, alisema mchakato wa upigaji kura hadi asubuhi saa 3.00 alipozungumza na Mwananchi, ulikuwa mzuri.

Alisema atakubali matokeo iwapo uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba ana uhakika wa kushinda kwa asilimia 70.

Mgombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Shaibu Akwilombe, ambaye alitarajiwa kupiga kura katika Kijiji cha Majimaji, alisema jana asubuhi kuwa ilikuwa mapema mno kutathimini hali ya uchaguzi kwa kuwa mchakato ni mrefu.

Akwilombe ambaye pia alikuwa na uhakika wa kushinda, alisema angekubali matokeo ikiwa taratibu za uchaguzi huo zingefuatwa.

Mazee na Akwilombe kwa nyakati tofauti walimshutumu Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Falhum Mshana kwa kauli yake ya kuwataka wananchi kurudi majumbani baada ya kupiga kura.

Walisema kauli hiyo inaingilia mamlaka yasiyokuwa yake na kwamba ni kinyume na sheria ya uchaguzi ambayo inawataka wapigakura kukaa umbali wa mita 200 kutoka katika kituo cha kupigia kura na si kwenda nyumbani.

Vile vile walisema aliyetakiwa kutoa maagizo hayo si polisi bali Msimamizi wa Uchaguzi huo.

Msimamozi wa Uchaguzi huo, Iluminata Mwenda, alisema uchaguzi ulianza vizuri na hadi saa 4.00 asubuhi alikuwa hajapokea taarifa zozote za matatizo.

Matokeo ya uchaguzi huo yalitarajiwa kuanza kutolewa jana jioni kwa wasimamizi wa vituo kubandika ukutani matokeo ya kila kituo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.