Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ofisi ya DC kuvunjwa kupisha uchimbaji dhahabu
Ofisi ya DC kuvunjwa kupisha uchimbaji dhahabu
By Habari Tanzania | Published  03/18/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Christopher Nyenyembe, Chunya

OFISI ya Mkuu wa Wilaya (DC) ya Chunya na ile ya halmashauri ya wilaya hiyo, zinaweza kubomolewa wakati wowote endapo wawekezaji waliomilikishwa eneo hilo na kupewa vibali vya kuchimba dhahabu wataamua kuanza kazi hiyo.

Siri hiyo kubwa iliyokuwa imejificha kwenye mioyo ya viongozi wa serikali kwa muda mrefu, ilifichuliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Noel Chiwanga.

Chiwanga aliamua kuweka hadharani donge alilokuwa nalo moyoni kwa muda mrefu alipozungumza wakati wadau wa mazingira walipokuwa wakijadili mchango wa sekta ya madini kwa ajili ya maendeleo ya jamii na athari zake kwa mazingira.

Chiwanga alisema kuwa, maeneo mengi yakiwemo yale ya vijijini, yanadaiwa kumilikishwa kwa raia wa kigeni na Wizara ya Madini, jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya watu na shughuli zao.

“Mwenyekiti wa NEMC, Mama (Hilda) Ngoye, hata hapa tunapofanyia mkutano huu, ofisi ya halmashauri ya wilaya na zile za mkuu wa wilaya, ramani za Wizara ya Madini zinaonyesha tayari ni mali ya watu,” alisisitiza mwenyekiti huyo wa halmashauri.

Alisema kwa mujibu wa ramani hiyo ya wizara, viwanja hivyo vimekuwa vikibadilishwa kwa wamiliki tofauti kupitia makao makuu ya wizara bila hata wahusika kujua hali hiyo.

“Inashangaza kuona kuwa watu wa madini wamekuwa wakibadilisha umiliki wa viwanja kwa ajili ya uchimbaji madini bila hata kufika Chunya na kujua hali halisi

Ilivyo, jambo ambalo ni la hatari… sijui sheria za madini zikoje,” alisema Chiwanga.

Alisema maamuzi kama hayo yanaweza kusababisha mgogoro mkubwa kati ya wawekezaji na serikali, kuhusu uhalali wa umiliki wa ardhi kutokana na mvutano wa kisheria utakaojitokeza iwapo wawekezaji hao watataka kufanya kazi katika maeneo hayo.

Baadhi ya madiwani waliochangia hoja katika mjadala huo, waliitaka serikali kuacha tabia ya kutowashirikisha wadau, hasa halmashauri, katika masuala nyeti yanayogusa maisha ya wananchi na kuitazama kwa undani Wizara ya Madini.

Walisema hali hii haionyeshi dhana ya uwajibikaji na utawala bora, wakirejea pia sheria za madini zinazokataza wananchi kuhoji wawekezaji katika sekta hiyo pale wanapoingia wilayani na kufanya mambo yasiyokubalika.

Akijibu baadhi ya michango iliyotolewa na wadau hao wa mazingira, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Hilda Ngoye, alisema jambo hilo linapaswa kupatiwa ufumbuzi wa haraka na serikali.

Ngoye alisema baadhi ya sheria zilizopo zinakanganya watu na zinafaa zipelekwe tena bungeni ili zifanyiwe marekebisho.

“Sheria hii ya madini inaonekana kuwa na mapungufu na hivyo kusigana na wizara nyingine kama vile ardhi, kilimo, maji na maliasili kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira, ikiwemo tathimini ya athari za mazingira katika maeneo ya machimbo,” alisema Ngoye.

Wajumbe wa bodi ya NEMC jana walihitimisha ziara yao ya siku sita mkoani Mbeya, ambapo walizitembelea wilaya nne za Mbozi, Ileje, Chunya na Mbarali.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.