Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Aua mke, mtoto kwa kuwachinja
Aua mke, mtoto kwa kuwachinja
By Habari Tanzania | Published  05/14/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
MKAZI wa kijiji cha Nkundi wilayani Nkasi, Lucas Simba (54) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchoma kisu mke wake na kumchinja mtoto wake wa kambo.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Germanus Mponguliana, aliwataja waliouawa kuwa ni Daudi Mapunda (mwenye umri wa miezi minne), ambaye ni mtoto wa kambo wa mtuhumiwa, na mkewe, Pili Ulungu (40) ambaye alimuua kwa kumchoma kisu tumboni hadi kufa.
 
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kaimu Kamanda ilieleza kuwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni usiku kwa kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi.
 
Ilielezwa kuwa Simba kabla hajafanya mauaji hayo alikuwa na ugomvi na mkewe, baada ya kurejea nyumbani na kuanza kumpiga mke wake, akachukua kisu kilichokuwa mezani na kumchoma kwenye titi la kushoto, hali iliyosababisha kutokwa na damu nyingi na kufariki dunia.
 
Mtoto katika mazingira hayo alianza kulia kwa kupiga kelele, hatua iliyomfanya mtuhumiwa kumkamata, akampiga kofi, na baada ya kuanguka alimwinua, na kuanza kumchinja kwa kutumia kisu ambapo alitenganisha kichwa na kiwiliwili.
 
Habari zaidi zinadai kuwa Simba wakati akimalizia kumchinja mtoto majirani walitokea na akatimua mbio.
 
Majirani walimkimbiza, akaingia kichakani, akazingirwa ndipo alipokurupuka na kumrukia mmoja wao na kumchoma kwa kisu tumboni na kumwacha utumbo ukining'inia nje.
 
Mponguliana alimtaja aliyjeruhiwa kwa kuchomwa kisu tumboni kuwa ni Joseph Lupia (20), mkazi wa kijiji hicho, ambaye amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi kwenye hospitali ya serikali ya mkoa wa Rukwa.
 
Kuona hivyo wanakijiji walitumia nguvu za ziada na kufanikiwa kumkamata Simba, ambapo inaelezwa kuwa kwa kutumia kisu kile kile alichofanyia mauaji walimkata sikio la kulia na kumjeruhi mikono yote miwili, na baadaye kumpeleka kituo cha polisi.
 
Simba anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa kujibu tuhuma zinazomkabili.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.