Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wawekezaji Bulyanhulu wasalimu amri kwa wenyeji
Wawekezaji Bulyanhulu wasalimu amri kwa wenyeji
By Habari Tanzania | Published  03/14/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu, Kahama

MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu umeanza kuifanya marekebisho barabara iliyosababisha machafuko baina ya mgodi na wananchi waiishio karibu na eneo hilo.
  
Katikati ya mwezi, uliopita mgodi huo ulimwaga kifusi katika barabara husika, ambapo wakazi wa karibu hususani wa Kijiji cha Kakola walikilalamikia kifusi hicho, wakidai kwamba kilikuwa na kemikali zinzoweza kudhuru afya zao.
  
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Barrick Tanzania inayomiliki mgodi huo, Sauda Kilumanga, alisema tayari wameanza kurekebisha barabara hiyo kama walivyokubaliana na Serikali.
  
Alisema marekebisho yanayofanywa ili kuondoa kifusi kilichomwaga awali, hayana maana ya kuthibitisha madai ya wakazi husika, bali uongozi wa mgodi uliona hakuna sababu ya kulumbana na wakazi hao bila sababu za msingi.
  
Alifahamisha kuwa migodi yote inayomilikiwa na kampuni hiyo nchini inazingatia kwa kiasi kikubwa uhifadhi wa mazingira, hivyo isingekuwa rahisi kwao kumwaga kifusi chenye kemikali katika makazi ya watu.
  
Alisema kutokana na kuzingitia uhifadhi wa mazingira, mara kadhaa wamekuwa wakitunukiwa tuzo mbalimbali katika hilo, kitu kinachothibitisha kuwa wako makini katika hilo.
  
“Tumeanza kuifanyia kazi barabara iliyokuwa inalalamikiwa katika kuondoa malumbano yasiyo na msingi, lakini haimaanishi kuwa madai yao kwamba tulimwaga kemikali yana ukweli,” alisisitiza Kilumanga.
  
Siku chache baada ya kumwaga kifusi hicho, wakazi husika hususani wa kijiji cha Kakola walilalamika kuwa walikuwa wanakohoa sana na huku wakudai kwamba hali hiyo imesababishwa na vumbi lililotokana na kifusi kilichomwaga katika barabara hiyo.
  
Katika kushinikiza kifusi hicho kuondolewa, wakazi walifunga barabara zinazotoka na kuingia mgodini hapo na kusababisha uzalishaji kusimama mgodini hapo hadi serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ilipoingilia kati, kwa Naibu Waziri wake kwenda huko na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.