Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Rais Kikwete awaangukia wawekezaji kutoka nje
Rais Kikwete awaangukia wawekezaji kutoka nje
By Habari Tanzania | Published  03/13/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na David Frank, Arusha

RAIS Jakaya Kikwete, jana aliwaangukia wawekezaji kutoka nje na kuwataka kuwekeza nchini ili kuisaidia serikali yake kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.

Alisema serikali inatambua umuhimu wa wawekezaji na ndiyo maana imekuwa ikiweka vivutio na kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji kutoka nje kuja nchini kufanya biashara kwani dhima kuu ni kukuza uchumi wa taifa.

Rais alisema hayo jana katika Hoteli ya kitalii ya Ngurdoto iliyoko nje kidogo ya Jiji la Arusha wakati akifungua mkutano wa sita wa Wawekezaji wa Kimataifa (IIRT), ambao umeandaliwa na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).

Mkutano huo ni mfululizo wa mikutano iliyoanzishwa na serikali kwa madhumuni ya kujadiliana masuala muhimu ya kiuchumi na wadau baada ya Tanzania kuondokana na mfumo wa uchumi hodhi.

Katika kuhakikisha dhima hiyo inafanikiwa, Rais Kikwete aliainisha sekta ambazo zitapewa kipaumbele katika kuboreshwa. Sekta hizo ni utalii, viwanda, kilimo, teknolojia ya mawasiliano na miundombinu.

Akizungumzia sekta ya utalii, Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa TNBC, alisema sekta hiyo itaendelea kupewa kipaumbele kwa kuwa inaliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

Alisema kuwa nchi ina vivutio vingi ambavyo wawekezaji wanayo fursa kubwa ya kuwekeza na kupata faida.

Akizungumzia sekta ya teknolojia ya mawasiliano, alisema sekta hiyo ni muhimu kwani ndiyo kiungo cha kurahisisha maendeleo, akibainisha kuwa pasipo na mawasiliano, mchakato wa maendeleo unakuwa mgumu.

“Tanzania itabidi kubadilisha kilimo chake kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji. Lakini kwa vile kilimo hicho kina gharama, hivyo nchi inahitaji wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta hiyo, kwani nchi yetu haina uwezo wa kumudu gharama hizo kwa wakati huu,” alisema.

Mkutano huo wa siku moja, ulihudhuriwa na makampuni 33 kutoka nje ya nchi, wakiwamo maofisa watendaji wakuu na wawekezaji wa kimataifa, akiwamo Mfaume Karim Aga Khan. Wengine ni Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, mabalozi na mawaziri.

Awali, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alisema azima ya serikali kwa sasa ni kuimarisha na kukuza ushirikiano na wawekezaji na akawahimiza wawekezaji hao kufanya kazi kama timu moja ili kufikia lengo la kukuza uchumi wa nchi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.