Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wadai posho kujadili wakopaji wa bilioni ya JK
Wadai posho kujadili wakopaji wa bilioni ya JK
By Habari Tanzania | Published  03/10/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Patrick Mabula, Kahama

WAJUMBE wa Kamati za Maendeleo ya Kata (WDC), wilayani Kahama, wamegoma kuhudhuria vikao vya kuwajadili wakopaji wa sh bilioni moja iliyotolewa na Rais Kikwete hadi watakapolipwa posho za vikao hivyo.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Tawi la Benki ya NMB, Kahama na kuthibitishwa na Meneja wa tawi hilo, Leon Ngowi, zilisema vikao vya kuwathibitisha waombaji kutoka katika kata vimekwamisha utoaji wa Fedha hizo.

Ngowi, alisema fomu za waombaji zimejazana katika benki hiyo lakini mihutasari na barua za kuwathibitisha waombaji hazijawasilishwa kutoka kwenye kata, kutokana na taratibu zilizowekwa na benki hiyo kushindwa kutoa pesa hizo.

Alisema pamoja na kuwa pesa hizo zipo tayari lakini benki hiyo inasubiri vikao vya WDC ili kupata uthibitisho wa walioomba na maeneo yao ya biashara kutambuliwa na wajumbe wa kamati hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati za maendeleo za kata ambao hawakupenda kutaja majina yao walisema hawezi kukaa hadi watakapolipwa posho za vikao vya kujadili maombi hayo ya wajasiriamali wanaotaka kuchukua hiyo bilioni ya Kikwete.

Aidha, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kahama, Ofisa Ushirika Marco Nzingura, alisema pesa hizo za mikopo haziwezi kutumika kuwalipa posho wajumbe.

Awali Tanzania Daima ilibaini kuwa fomu za kuomba mkopo huo zinauzwa kati ya sh 2,000 hadi sh 5,000 kwa wale wanaozitafuta.

Aidha, waombaji hao wamelalamikia kukatwa kati ya sh 5,000 hadi sh 20,000 kwa ajili ya mchango wa sekondari za kata.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.