Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Jeuri za nduguze Dito sasa zageuka kidonda
Jeuri za nduguze Dito sasa zageuka kidonda
By Habari Tanzania | Published  03/10/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu

SIKU moja baada ya polisi, ndugu na jamaa wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kuanzisha vurugu, kutoa maneno ya kejeli na mbwembwe zisizo na msingi katika eneo la Mahakama Kuu, Jeshi la Polisi limeiomba radhi Mahakama Kuu.

Limesema linatambua kuwa kitendo kilichofanywa na askari wake cha kumpitisha Ditopile mlango wa nyuma wa mahakama, isivyo kawaida, kimeleta usumbufu mkubwa kwa uongozi wa mahakama.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya dare s Salaam, Alfred Tibaigana alisema jeshi hilo limeanzisha uchunguzi ili askari waliohusika na kitendo hicho waweze kuchukuliwa hatua baada ya kugundua kuwa mlango huo hutumiwa na majaji tu wanapoingia na kutoka kazini.

Tibaigana aliwaonya ndugu wa Ditopile kuachana na vitendo vya ubabe kama walivyovionyesha katika Mahakama Kuu juzi, kwa sababu vinaweza kujenga picha mbaya kwa jamii.

Alisema umma ulitegemea ndugu wa mtuhumiwa huyo kuwa watu wa masikitiko zaidi na kumuombea dua ndugu yao kuliko vitendo walivyovifanya.

“Katika hali ya kawaida ningetegemea ndugu zake na Ditopile kuwa katika hali ya utulivu na pengine wengi wao kubaki nyumbani wakiomba dua, kwani si rahisi kufahamu mahakama ingeamua vipi…lakini haikuwa hivyo, ndugu wa mtuhumiwa huyo walionyesha vitendo vya kibabe, na hii ni picha mbaya,” alisema Kamanda Tibaigana.

Aliwataka ndugu wa mtuhumiwa huyo kujirudi kwa vile polisi hawana nia ya kuonyeshana ubabe na familia hiyo.

Alisema polisi wanaamini kuwa iwapo itatumika nguvu kubwa katika kushughulikia ulinzi wa mtu mmoja kwa sababu ya ubabe wa ndugu zake, jambo hilo litaacha maswali mengi kwa wananchi.

Tibaigana alitumia nafasi hiyo kuwapa pole waandishi wa habari ambao vifaa vyao viliharibiwa baada ya vurugu kuanza katika eneo hilo la Mahakama Kuu.

Alisema wingi wa waandishi wa habari na kutokuwa na alama maalumu ya kuwatambua kuliwafanya polisi washindwe kuwatofautisha na ndugu zake Ditopile, hivyo vurugu zilipoanza, polisi walishindwa kuwalinda baada ya kuwa wako njia panda.

Akizungumzia uamuazi wa vijana wake kumpitisha mtuhumi huyo mlango unaotumiwa na majaji, alisema waliamua hivyo kwa ajili ya kulinda usalama wake, kwa sababu mlango wa mbele ulikuwa umefurika watu.

Wakati Jeshi la Polisi likitamka hayo, baadhi ya wanaharakati na wanasiasa, jana walizungumza na waandishi wa habari katika nyakati tofauti na kueleza kutoridhishwa na utendaji kazi wa polisi na pia kukerwa na vitendo viliyofanywa na ndugu na jamaa wa Ditopile.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Helen Kijo-Bisimba, alitoa kauli ya kulaani vurugu hizo na kueleza kuwa si kitendo cha ustaarabu, hakivumiliki na hakiwezi kupita bila kukemewa.

“Tunalaani vitendo vya vurugu dhidi ya wanahabari na vitendo vya kudharau mahakama vilivyofanywa na polisi wakisaidiana na jamaa wa mshitakiwa. Hali kadhalika tunaeleza kufurahishwa kwetu na jinsi mtuhumiwa Ditopile alivyopewa huduma nzuri za usafiri na ulinzi pamoja na upelelezi wa kesi yake kwenda haraka.

“Kwa kuwa tunaamini kuwa watuhumiwa kama yeye wa kesi za mauaji wako wengi wakiwamo waliokaa mahabusu kwa zaidi ya miaka 10 wakisubiri hatima ya kesi zao, tunatoa mwito kwa vyombo vya dola kuhakikisha kuwapo dhamana kwa watuhumiwa, huduma nzuri za usafiri wa kwenda mahakamani na ukamilishaji wa upelelezi wa haraka kama ilivyokuwa kwa kesi ya Ditopile, ili kuondoa hisia kuwa kuna raia wa madaraja tofauti,” alisema Bisimba.

Bisimba alisisitiza kuwa ni aibu kwa chombo kinachoaminika kama polisi kutenda kitendo kinachodhalilisha heshima ya Mahakama, na uthibitisho wa kiwango cha juu wa kutoogopa mamlaka na kumomonyoka kwa misingi ya utawala wa sheria.

Sambamba na Bisimba, Baraza la Habari Tanzania (MCT), limemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika na unyanyasaji na matumizi ya mabavu dhidi ya waandishi wa habari.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Anthony Ngaiza, alitangaza uamuzi huo wa baraza jana wakati akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya baraza hilo.

Alisema baraza lilifanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo jana asubuhi na kubaini waandishi walikuwa wanafanya kazi zao katika maadili, lakini polisi waliokuwa katika eneo hilo walitumia mabavu kuwashambulia wanahabari hao ili wasitekeleze majukumu yao.

Ngaiza alisema, kama Jeshi la Polisi, linatakiwa kufanya kazi yake kwa uadilifu, bila kutumia mabavu dhidi ya waandishi, hivyo IGP anatakiwa kuwawajibisha askari waliohusika katika tuhuma hizo.

“MCT limesikitishwa na kushangazwa na vitendo vya unyanyasaji huo, kitendo hicho ni fedhea kwa Mahakama Kuu, mtuhumiwa kupitishwa katika mlango wa majaji, eti askari hawajui, wakati kila siku wako mahakamani, hii nini maana yake,” alisema Ngaiza.

Alisema matukio ya juzi, ni mlolongo wa vitendo ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na jamaa zake, Ditopile, lakini wanakosa msaada kutoka kwa askari wanaokuwa katika uangalizi wa kulinda usalama mahakamani.

“Wakati Baraza na Jeshi la Polisi vimekuwa katika harakati za kujenga mahusianao mazuri ya utendaji kazi kati ya waandishi na polisi, limesikitishwa kuona vitendo ambavyo polisi wanashiriki katika kuzuia waandishi wasifanye kazi zao na kuwalinda wanaowanyanyasa na kuwafanyia fujo,” alisema Ngaiza.

Ngaiza aliwataka waandishi wote waliopigwa, kuorodhesha majina yao na mali walizopoza, na kufika katika ofisi za MCT ili kufanya utaratibu wa kupata haki zao zilizopotea.

Naye Mwenyekiti wa Democratic Party (DP) Christopher Mtikila, ametoa saa 24 kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, kuwafikisha mahakamani askari waliohusika katika vitendo vya vurugu mahakamani.
Alisema iwapo Kamanda Tibaigana hatatekeleza kauli hiyo, yeye (Mtikila) atamshitaki mahakamani kwa sababu kitendo kilichofanywa na polisi ni kosa la jinai.

Mtikila alisema ulinzi aliopewa Ditopile jana unaonyesha kuwa polisi na ndugu zake walikuwa wakimkinga asionwe na umma kwa sababu ya kosa alilolitenda la kumuua mwanachi asiye na hatia.

“Waandishi wa habari walipaswa kuuambia umma wa Watanzania na ulimwengu mzima kwa jumla juu ya tukio hili kwa sababu ya uzito wake, kazi ya wanahabari ni utekelezwaji wa matakwa ya Katiba ya nchi, tangazo la ulimwengu la haki za binadamu, uhuru na heshima ya mahakama kwa ajili ya utawala bora unaohimizwa na ulimwengu kwa sasa,” alisema.

Alisema kitendo cha kumpitisha Ditopile mlango unaotumiwa na majaji na kumpiga kikumbo ofisa wa mlangoni ni kosa zito la uharamia na kuidharau mahakama.

“Nashangaa kuona muuaji akipewa ulinzi mkubwa kama muungwana na kupitia mlango wa nyuma unaotumiwa na majaji, inaonyesha kwamba alipewa ulinzi wa dola wa Rais Kikwete, jambo ambalo halijawahi kutokea hapa nchini,” alisema Mtikila.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Tanzania Daima kuhusu tukio hilo, walisema kauli za ndugu zake Ditopile zinaonyesha dhahiri kuwa haki haiwezi kutendeka katika kesi hiyo.

Mmoja wa watu waliozungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema majigambo ya ndugu zake Ditopile kuwa ilikuwa ni lazima aachiwe kwa kuwa ni rafiki wa wakubwa serikalini (best man) wa Rais Kikwete, inadhihirisha kuwa maskini katika nchi hii, haki yake ni kifo dhidi ya jamaa na ndugu wa rais.

Kauli hizi za wanaharakati na wananchi wa kawaida, zinatokana na vitendo vya vurugu, kejeli na mbwembwe zilizofanywa jana na ndugu na jamaa wa Ditopile kwa kusaidiwa na polisi dhidi ya waandishi wa habari.

Katika vurugu hizo, waandishi kadhaa walijeruhiwa na wengine kuharibikiwa vitendea kazi vyao, zikiwemo kamera, zilizoambatana na kurushiana makonde na maneno kati ya wanahabari hao kwa upande mmoja na jamaa na ndugu wa Ditopile kwa upande mwingine.

Vurugu hizo ziliambata na vitendo vya kuwamwangia maji wanahabari na kutoa maneno ya kuidharirisha serikali na hata viongozi wake wakuu jambo lililoonyesha jinsi wasivyokuwa na staha, wasivyojiheshimu, walivyopungukiwa hekima, wasio kuwa na subira na walioamua kwa makusudi kuidharau Mahakama na taaluma ya habari.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by AFRODIME)
    Rating
    AfroCentric Digital Media imesisikitiswha mno na kitendo cha unyanyaswaji kinachofanywa na vyombo vya Dola dhidi ya wanahabari nchini Tanzania. Tunatakiwa kubadilika na kupiga kona kwa kutoka Bagamoyo Mkuranga na Rufiji kuelekea ulimwengu w kisasa. Polisi inatkiwa kufanya kazi yake bila kujali huyu anatoka wapi na ndugu zake wako wapi. Nawapa Pole wanahabari wenzetu wa Tanzania wanaopatwa na shida hizo. AFRODIME itatoa Press Release siku ya Jumatatu kutokana na tukio hilo
    www.afrodime.com
     
Submit Comment


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.