BAGHDAD, Iraq
ASKARI wanne wa Iraq wameshtakiwa kwa kumbaka mwanamke wa Kabila la Kisunni katika eneo la Talafar Kaskazini mwa Iraq, maafisa wamesema.
Washtakiwa hao wamekiri kubaka na hii ni mara ya pili kwa askari wa Iraq kuwabaka wanawake wa Kabila la Kisunni.
Generali Abdullah alisema amepokea malalamiko ya Wasunni kuhusiana na kundi la askari hao kuwa waliingia kwenye nyumba ya mwanamke huyo na kumbaka.
"Mmoja wa askari jina lake Mushtaq Taleb kutoka Basra. Alitaka kuwatisha kwa silaha waache nia yao lakini walimbaka ...," alisema Generali Abdullah.