WATU zaidi ya 600 wamekamatwa na polisi nchini Sweden katika mfulilizo wa maadamano ya vurugu ya siku tatu ya kupinga kuondolewa kwa nguvu katika jengo linalotumika kwa biashara mjini Copenhagen, Sweden.
COPENHAGEN
WATU zaidi ya 600 wamekamatwa na polisi nchini Sweden katika mfulilizo wa maadamano ya vurugu ya siku tatu ya kupinga kuondolewa kwa nguvu katika jengo linalotumika kwa biashara mjini Copenhagen, Sweden.
Maandamano hayo yalianza baada ya vijana na watu wengine kuondolewa katika jengo hilo kwa amri ya mahakama ambalo linatumika kwa shughuli za biashara.
Wanaharakati wa mlengo wa kushoto wamekuwa wakitetea eneo hilo tangu mwaka 1982, lakini mwaka 2000 Jiji la Copenhagen liliuza eneo hilo kwa kundi moja la kikristu.
Baada ya kuuziwa, kundi hilo lilipata kibali cha mahakama cha kuwaondoa watu hao lakini wanaharakati wamekuwa wakiwashawishi wasiondoke kwa kuwa Serikali haina haki ya kuuza jengo hilo kwa sababu bado lilikuwa likitumika.
Katika maandamano hayo, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na mabomu ya kurusha kwa mkono ya petroli ili kuwatawanja waandamanaji hao.
"Miaka 10 iliyopita, hatujawahi kuona maandamano kama tuliyoyaona miaka miwili iliyopita," alisema msemaji wa polisi wa Copenhagen, Flemming Steen Munch.
Ilielezwa kuwa katika vurugu hizo, licha ya unaribifu mkubwa kutokea ni watu wawili tu waliojeruhiwa.
Polisi ilisema kati ya watu waliokamatwa, wengi wao ni Wajerumani, Wanorway na Wsweden.
Wanasisasa wa mlengo wa kushoto wakizungumza katika maandamano hayo, waliwaomba wanaharakati hao kusimamisha vurugu hizo. Watu 2,000 walishiriki katika maandamano hayo.