Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Jeshi la Israel latumia watoto kujihami
http://www.habaritanzania.com/articles/3259/1/Jeshi-la-Israel-latumia-watoto-kujihami
By Habari Tanzania
Published on 03/10/2007
 
MAKUNDI ya haki za binadamu nchini Israel, yamelishitumu jeshi la Israel kwa kuwatumia watoto wadogo wawili wa Kipalestina kama ngao ili kujizuia na mashambulizi yalitokea katika eneo la Ukingo wa Magharibi.

NABLUS, Jerusalem

Makundi hayo, yalisema kuwatumia watoto hao kama ngao ni kinyume na sheria za Israel na zile za kimataifa. Jeshi la Israeli, limesema litachunguza madai hayo.

Jeshi la Israel, limeushikilia mji wa Nablus kwa muda wa siku tano sasa kwa ajili ya kuyasaka makundi ya wanamgambo na kukusanya silaha.

Wanajeshi hao, wanafanya upekuzi wa nyumba hadi nyumba na wametangaza amri ya hatari ambayo itadumu kwa muda wasiku mbili.

Vijana hao, cousin Samah (24) na  Amid Omeira (15), walisema wanajeshi hao, waliwalazimisha kuingia katika nyumba moja iliyokuwa mbele yao ili waweze kujikinga na mashambulizi yaliokuwa yakifanywa na wanamgambo.