SAO PAOLO
RAIS wa Marekani George W. Bush amepokelewa kwa maandamano yalioambatana na vurugu nchini Brazil kutokana na Marekani kuivamia Iraq na kusababisha vita nchini humo.
Katika ziara yake hiyo, wananchi wa Brazil walisema kuwa hawamtaki Rais Bush nchini kwao kwa sababu alianzisha vita Iraq na kwamba ameenda Sao Paolo kwa ajili ya kusimamia uzalishaji wao wa nishati ya gesi.
Rais Bush aliwasili Brazil ili kukutana na Rais wa nchi hiyo, Luis Inacio Lula da Silva kwa kelengo la kusaini mkataba wa pamoja wa nishati. ethanol energy alliance.
Katika maandamano hayo, watu wasiopungua 20, walijeruiwa
wakati polisi walipokuwa wakijaribu kuwathibiti waandamanaji hao.
Maandamano hayo, yalihusisha vurugu baada ya waandamanaji kurusha mawe, nyanya na vitu vingine huku wanajeshi 4,000 wakiwa wanalinda usalama mara baada ya Rais Bush kuwasili.
Kutokana na vurugu hizo, polisi walijibu mashambulizi hayo kwa kupiga bomu la machozi ili kutuliza ghasia.
Rais Bush atatembelea pia Uruguay, Colombia, Guatemala na Mexico katika ziara yake itakayomchukua wiki moja.
Together with Colombia, Brazil produces about 70% of the world's ethanol, a bio-fuel made from sugar cane or corn.