Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yasisitiza mabilioni ya Kikwete siyo sadaka,ruzuku
Serikali yasisitiza mabilioni ya Kikwete siyo sadaka,ruzuku
By Habari Tanzania | Published  03/10/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema Sh21 bilioni zilizotolewa kusaidia kupambana na umaskini nchini siyo ruzuku wala sadaka, bali fedha za walalahoi zinazotakiwa kukopwa kwa nidhamu ili itimize malengo.

Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chiligati, alisema jana katika taarifa yake kuwa wakopaji wa fedha hizo wanatakiwa kufuata taratibu zilizowekwa na benki katika upatikanaji wake kuepuka usumbufu usio wa lazima.

"Wito wa serikali ni kwamba fedha inahitajika nidhamu ya kukopa na kurejesha. Sio fedha za ruzuku wala sadaka. Na pia hakuna njia ya mkato wala ujanja, wakopaji wote lazima wafuate utaratibu uliowekwa na serikali," alisema Waziri Chiligati

Alisema masharti yaliyowekwa na benki za NMB na CRDB katika upatikanaji wa mkopo huo, yamelenga kudhibiti fedha hizo zisije zikaingia katika mikono ya wajanja na kama kuna udhaifu katika masharti hayo, utafanyiwa marekebisho kadri muda unavyokwenda.

"Utaratibu huu ni mpya kwa kila mtu, yaani kwa viongozi na serikali, maafisa wa benki na wajasiriamali. Hivyo mwaka huu wa kwanza lazima tupate matatizo na vikwazo vingi. Lakini kwa kuwa mfuko huu ni endelevu, kila upande utaendelea kujifunza na kujirekebisha," alisema Chiligati.

Alisema fedha hizo zimetolewa kwa lengo la kupambana na umaskini na zitaendelea kutolewa kila mwaka zikiwa zimepunguziwa masharti ili kuwawezesha wajasiriamali walengwa kuzipata.

Februari 22, mwaka huu, serikali ilifanya mazungumzo na benki za CRDB na NMB zilizopewa dhamana kutoa mikopo huu na kuzitaka zilegeze masharti kufungua mlango kwa walengwa kuzipata.

Kwa mujibu wa Chiligati, kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu Edward Lowassa, kiliitaka benki ya NMB kuondoa masharti ya dhamana, namba ya mlipakodi (TIN) namba na leseni ya biashara na kupunguza sharti la muda wa biashara ya mwombaji kuwa ya kuanzia kipindi cha mwaka mmoja.

Alisema benki hiyo sasa pia itatoa mikopo kwa wakulima na wafugaji ambao watatakiwa kurudisha fedha hiyo kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu.

Chiligati alisema tangu kuanza kutolewa kwa fedha hiyo Januari mwaka huu, benki ya NMB imeshakopesha jumla ya sh141.8milioni kwa wajasiriamali 101, wakati CRDB imetoa mikopo kwa wana Saccos 862 yenye jumla ya Sh190.5milioni.

Kauli hiyo ya Chiligati imekuja siku moja baada ya tamko la Rais Kikwete kuwa mabilioni hayo lazima yawe na masharti na akawataka wananchi kuyafuata ili kupata fedha hizo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.