Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kimataifa  »  Mawaziri Iraq matumbo joto, wahofia mabadiliko
Mawaziri Iraq matumbo joto, wahofia mabadiliko
By Habari Tanzania | Published  03/8/2007 | Habari za Kimataifa | Unrated

BAGHDAD

WAZIRI MKUU wa Iraq, Nouri al-Maliki amesema wiki mbili zijazo atafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri ili kumaliza mgawanyiko wa makundi ya kikabila katika Serikali yake na kuleta umoja wa kitaifa.

Waziri huyo aliliambia shirika la habari la AP kwamba atahakikisha Iraq inafanikiwa na kuwa usalama madhubuti.

Waziri Mkuu huyo, Al-Maliki umekuwa katika wakati mgumu hasa baada ya Marekani kumshinikiza kumaliza mgawanyiko ulioko katika ya serikali iliyowashirikisha Wahiite, Wasunnina Wakurd.

Al- Maliki hakusema ni mawaziri wangapi katika baraza lake watabadilishwa lakini maafisa wa Serikali yake, walisema mawaziri tisa watapoteza kazi, wakiwemo mawaziri sita wa kabila la Shiite ambao wanaipinga Marekani.

Muqtada al-Sadr katika bunge la Iraq, ana viti 30 kati ya viti 275 vya bunge.

Hata hivyo pamoja na al- Sadr kuwa na viti vingi bungeni, Marekani imekuwa ikimshawishi Waziri Mkuu, al-Sadr kuachana na al- Sadr na kuunda muungano mpya wa Washiite, wakimo Wasunni wachache na Wakurd.

Ilielezwa mkutano utakaofanyika wiki ijayo, utawaunganisha Wairaq wote, Iran na Syria pamoja na nchi za magharibi.

Hata hivyo Iran haijathibitisha kama itaudhuria mkutano huo au la lakini Iraq inaamini Tehran itamtuma mwakilishi wake.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Favourites' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.