Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kesi ya uchaguzi Tunduru yaiva
Kesi ya uchaguzi Tunduru yaiva
By Habari Tanzania | Published  03/7/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, itaanza kusikiliza kesi ya kikatiba ya kusitishwa kwa maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tunduru, utakaofanyika Machi 18, mwaka huu.

Kesi hiyo namba 19 ya mwaka 2007, ilifunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Christopher Mtikila, wiki iliyopita dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Othman Chande, Jaji Robert Makaramba na Jaji Amir Mruma, waliutaka upande wa wadaiwa kuwasilisha hoja zao Ijumaa ya wiki hii.

Aidha, upande wa mlalamikaji umetakiwa kujibu hoja hizo na kuziwasilisha mahakamani hapo Jumatatu ijayo. Wadaiwa wanatetewa na Wakili wa Serikali Mathew Mwainu, wakati Mtikila anatetewa na wakili wa kujitegemea Mpare Mpoki.

“Mahakama imesikiliza hoja zenu na hivyo maagizo mliyopewa ni lazima yatekelezwe kwa wakati ili Jumanne ijayo kesi ianze kusilikizwa…nasisitiza utekelezaji wa maagizo hayo,” alisema Jaji Othman Chande.

Jumatatu iliyopita, Mtikila alifungua kesi mahakamani hapo chini ya hati ya kiapo cha dharura, akitaka mahakama isitishe maandalizi ya uchaguzi wa Jimbo la Tunduru, kwa kuwa unakwenda kinyume cha Katiba ya Jamhuri na uamuzi wa Mahakama.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Mtikila, anadai kwamba tamko la mdaiwa wa kwanza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), ambaye alitamka hivi karibuni kwamba wagombea binafsi hawaruhusiwi kushiriki katika uchaguzi katika jimbo hilo ni batili.

Anadai kuwa tamko hilo linakwenda kinyume cha Ibala ya 20(4), 2(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.