Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mke, mume kizimbani kwa kudhulumu yatima
Mke, mume kizimbani kwa kudhulumu yatima
By Habari Tanzania | Published  03/6/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Asha Bani

EDITH Kahanda na Deo Kahanda, ambao ni mume na mke, wakazi wa Ilala, jijini Dar es Salaam, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakituhumiwa kuuza nyumba ya mirathi kwa sh milioni 115 na kuwadhulumu watoto watatu wa marehemu, Juma Abdallah.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Kahanda na mkewe, waliuza nyumba hiyo kwa makubaliano kwamba watawagawia watoto hao fedha hizo lakini hawakufanya hivyo.

Watoto waliodhulumiwa walitajwa kuwa ni Seif Jumbe, Rehema Mashaka na Nusura Abdallah, ambao walidai kuwa kulikuwa na makubaliano ya kulipwa kila mrithi kiasi sawa cha fedha, lakini ikatokea kinyume baada ya waliompendekeza kuwa msimamizi wa mirathi, Edith, kuwadhulumu.

Watoto hao walidai kuwa, Edith aliwaahidi kuwagawia fedha hizo katika kipindi cha wiki mbili tangu kuuzwa kwa nyumba hiyo.

Walidai kuwa wiki mbili zimepita na hawajapatiwa fedha, walifungua shitaka la madai katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni, ambayo awali ndiyo iliyomuidhinisha Edith kuwa msimamizi wa mirathi.

Alipofikishwa mahakamani hapo, Edith aliahidi kutoa fedha hizo mara ifikapo Januari 31 mwaka huu. Hata hivyo, hakutoa fedha hizo na watoto hao waliamua kulifikisha suasla hilo mahakamani hapo.

Watoto hao walidai kuwa wakati wanafuatilia fedha zao, mume wa Edith (Deo), aliamua kwenda mahakamani na kudai kuwa mkewe alimuingizia fedha hizo katika akaunti yake katika Benki ya NBC Tawi la Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, na kukiri kuzitumia fedha hizo pamoja na mkewe.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.