Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Anglikana wazozana na SMZ
Anglikana wazozana na SMZ
By Habari Tanzania | Published  03/6/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

MGOGORO mkubwa umezuka baina ya Kanisa la Anglikana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kuhusu umiliki wa Shule ya Msingi Mkunazini.

Sakata hilo limeibuka baada ya kanisa kudai halina imani na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman, baada ya kushindwa kuirejesha shule hiyo kwa kanisa kwa zaidi ya miaka mitano.

Katibu wa kanisa hilo Jimbo la Zanzibar, Nuhu Sallanya, alisema licha ya uongozi wa kanisa kukutana mara mbili na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, maazimio ya vikao hivyo hayajatekelezwa.

Alieleza kwamba, hivi sasa wameamua kumwandikia barua Rais Karume achukue hatua za kulitafutia ufumbuzi wa kudumu ombi lao la kutaka kurejeshewa shule hiyo ambayo ilikuwa mali ya kanisa kabla ya kutaifishwa na serikali baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Alisema kwamba katika kikao kilichohusisha marehemu Askofu Douglas Toto, pamoja na Rais wa Zanzibar, ilikubalika kuwa taratibu zifanyike kuhakikisha shule hiyo inarejeshwa kwa wahusika lakini hadi sasa hilo halijatekelezwa.

“Kazi iliyotakiwa kufanyika kwanza ilikuwa ni kuwahamisha wanafunzi kutoka katika majengo na kuwapeleka mahali pengine na kazi hiyo alikabidhiwa waziri anayehusika na elimu,” ilieleza barua hiyo.

Hata hivyo barua hiyo kwenda kwa Rais wa Zanzibar ilisema utekelezaji huo haujafanyika kwa muda wa miaka mitano na badala yake sehemu ya ardhi ya shule hiyo imekuwa ikijengwa majengo ya kudumu ya biashara.

“Wizara ya Elimu inafahamu fika mchakato huu, lakini kwa makusudi imeanzisha ujenzi wa maduka ya kudumu katika eneo letu.

“Si vyema kutupuuza kwa sababu ya uchache wetu ama sababu ya imani yetu,” inaongeza barua hiyo.

Uongozi huo wa kanisa umemtaka Rais kusitisha mara moja ujenzi wa maduka unaoendelea katika eneo la ardhi la shule hiyo, hadi hapo uamuzi utakapotolewa katika suala hilo.

“Hatua za makusudi zichukuliwe kuwahamisha watoto na kutukabidhi jengo na eneo letu,” alisema Sollanya.

Alisema kwamba shule hiyo hivi sasa inakabiliwa na hali mbaya ya uchakavu na hatua ya kurejeshwa itasaidia kufanyiwa matengenezo makubwa na kuendelea kutoa elimu kwa vijana mbali mbali.

Alieleza kwamba ni jambo la kushangaza kwamba shule iliyokuwa imetaifishwa kutoka Jumuiya ya Sunni Manzil, imerejeshwa kwa wahusika, lakini maombi ya kanisa kutaka shule yao nayo irejeshwe, hayajashughulikiwa hadi sasa.

“Tumeamua kulikabidhi suala hili kwa Rais baada ya kuona muda unakuwa mrefu na utekelezaji wake ni mdogo na eneo la ardhi limeanza kuvamiwa na wafanyabiashara,” alisema Sallanya.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, alithibitisha kuwapo kwa tatizo hilo, lakini alisema linashughulikiwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.