Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Msako wa wasomali Arusha waiva
Msako wa wasomali Arusha waiva
By Habari Tanzania | Published  03/5/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu, Arusha

ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kutoka jijini Dar es Salaam, wamewasili wilayani Ngorongoro jana kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kukabiliana na majambazi wa Kisomali waliovamia watalii na kuwanyang'anya fedha na mali mbalimbali.

Upelekaji wa kikosi hicho cha ziada umefanyika baada ya FFU wa mkoani Arusha wapatao 79 ,wanaondelea na msako wa Wasomali hao, kukabiliwa na changamoto ya ukubwa wa msitu wanamojificha majangili hao.

Habari za uhakika kutoka Ngorongoro, zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Matei Basilio, ambaye ameweka kambi Loliondo akishiriki msako dhidi ya majangili hao, zimeeleza kuwa tayari askari hao kutoka Dar es Salaam wameanza kazi.

Ukubwa wa mbuga na mapori katika wilaya hiyo ndiyo uliosababisha Kamanda Matei na Kamanda wa Kupambana na Wizi wa Mifugo Tanzania, Wencesilaus Magoha, kuzunguka katika vijiji vilivyopo mipakani kuhamasisha raia ili waote taarifa haraka pindi wanapowaona Wasomali katika maeneo yao.

Katika ziara hizo za kuhamasisha jamii juu ya utoaji taarifa za wahalifu kwa Jeshi la Polisi, makamanda hao wamekutana na changamoto za kuhitajika kwa askari katika vijiji hivyo na uanzishwaji wa vituo vya polisi ili kurahisisha mawasiliano.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wakitoa maoni yao kwa kamanda Matei, walisema Kituo cha Polisi katika Kijiji cha Malambo kina askari mmoja tu, hivyo hata watalii walipovamiwa na Wasomali hao, alishindwa kutoa msaada wowote.

Wakazi wa Kijiji cha Pinyinyi kilichopo katika mpaka wa Kenya na Tanzania kupitia kwa diwani wao, Charles Ndikere, walisema kukosekana kwa kituo cha polisi katika mpaka huo kumesababisha kijiji kuwa njia kuu ya Wasomali kuingia Tanzania kufanya uhalifu.

Ndikere alisema mpaka huo ulianza kutumiwa na Wasomali tangu 1998 wakati wakiingia nchini kufanya biashara ya kuuza shanga na chumvi kutoka Kenya na mwaka 2000 ambapo waliingia na kufanya mauaji ya Watanzania 9 katika Kata ya Malambo.

Alisema hali hiyo imewafanya Wasomali kuutambua udhaifu uliopo katika mpaka huo na kufanikiwa kuingia kirahisikwa kutumia mapori yaliopo katika mpaka huo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Kamanda Basilio aliwaahidi kutoa askari katika kijiji hicho ambao watashirikiana na mgambo kudhibiti mpaka na kuwahamasisha wananchi wajitolee kujenga kituo cha polisi.

Majangili wanne wa Kisomali wakiwa na silaha za kisasa, hivi karibuni waliwateka watalii na kuwapora mali na fedha. Ingawa bado hawajakamatwa, wamekuwa wakionekana katika vijiji kadhaa na baadhi ambako wamekuwa wakivamia maboma na kuchukua mbuzi kwa ajili ya chakula.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.