Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Vurugu zawatikisa Anglikani Mwanza
Vurugu zawatikisa Anglikani Mwanza
By Habari Tanzania | Published  03/5/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MGOGORO wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza, Mwanza, jana umeingia katika sura mpya baada ya Askofu John Changae anayedaiwa kuondolewa madarakani, kufunga milango ya kanisa ili kuwazuia baadhi ya waumuni kuingia kusali.

Vurugu hizo zilizuka jana katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicholas saa 2.47 asubuhi wakati ibada ya kwanza ilipokuwa ikiendelea, na waumini wengine wakikusanyika kwa ajili ya misa ya pili.

Huku askari kanzu wakiwa wametanda kila kona, na waumini wakiendelea kukusanyika kanisani hapo, Askofu Changae alifika nje ya kanisa akitokea kwake na kuanza kuamuru waumini wasiosali katika kanisa hilo kuondoka mara moja.

“Sitaki msalie hapa, ondokeni, nasema watu wote ambao huwa hamsali hapa muondoke… mnaleta vurugu mtoke,” alisema huku akipita huku na huko katika maeneo ya kanisa na akifuatwa na mwanawe, Kara Changae, ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza baba yale.

Hakuna muumini ambaye alimjibu, hadi akamwagiza mwanawe Changae kumletea funguo za kanisa na baada ya kuletewa, alianza kufunga milango ya pembeni mwa kanisa hilo na kuja kufunga mlango mkubwa, lakini waumini wakauvamia mlango huo kuuzuia usifungwe.

Hatua hiyo ilizusha mvutano baina ya askofu huyo na waumini huku mwanae Kara akiwa amekaa katikati ya malango mmoja akizuia waumini kuingia kanisani humo, hatua ambayo iliingiliwa na maafisa wa polisi waliokuwa eneo hilo na kuwasihi kutulia ili wazungumze na Askofu.

Mvutano huo ulimalizika majira ya saa 10.12 asubuhi baada ya maafisa wa polisi kukutana na Askofu huyo na kumsihi aruhusu waumini hao kusali kanisani hapo.

Alikubali kuondoka na kuwaacha waumini wakiingia kanisani kuendelea na ibada. Akizungumza na gazeti hili, Mchungaji Kanoni Jonas Ntete wa Igogo, alisema kuzuiwa kwa waumini hao katika kanisa lao ni kosa na kuongeza kuwa ibada
itaendeshwa hata chini ya mti kwa vile walikuwa wamekusudia kusali kutoa shukrani ya kumwondoa Askofu huyo katika kiti hicho.

Alisema licha ya Askofu Changae kung’ania madaraka, wao kupitia kikao chao cha Sinodi kilichoketi hivi karibuni wataendelea kusali katika kanisa hilo mpaka hapo watakapompata Askofu mwingine.

“Leo ilikuwa tukutane makanisa yote ya Jiji la Mwanza hapa tusali misa ya shukrani kumshukuru Mungu kumwondoa hapa askofu huyu, lakini kutokana na polisi kutusihi kulinda amani, tumelazimika kuwaomba waumini wa makanisa mengine kuendelea kusalia huko, imezua mvutano lakini tumesali kumshukuru Mungu,” alisema Mchungaji Ntete.

Askofu Changae ambaye baada ya jeshi la polisi kuingilia kati na kumwagiza kuondoka kuwapisha waumini hao kusalia hapo na kuondoka, alikataa kuzungumza na waandishi wa habari kwa madai kuwa siku ya kufanya hivyo bado haijafika.

“Siwezi kuongea sasa… naomba mnipishe siku ikifika nitawaita leo sitaki,” alisema Askofu huyo huku akitokomea katika makazi yake yaliyopo jirani na kanisa hilo na waumini wakiingia kanisani huku wakiimba wimbo wa ‘Yote yanawezekana’.

Ibada hiyo iliyoendesha na mchungaji Ntete, iliendelea ikiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.Juzi katika mkutano wa Sinodi wa Dayosisi hiyo, wajumbe walimwondoa madarakani Askofu Changae kwa madai ya kuhujumu mali za kanisa, kulifanya kama mali yake binafsi na kuleta mgawanyiko.

Katika mkutano huo ambao umedaiwa kuwa ndiyo wenye nguvu kikatiba kumwondoa askofu, mmoja wa wachungaji, Josiah Gachocha, alisoma tamko na kumtaka Askofu huyo kujiuzulu uongozi huo na pia kujianda kukabiliana na sheria kutokana na ufujaji wa mali za kanisa.

Akisoma taarifa hiyo, Mchungaji Gachocha alieleza kuwa tangu mwaka 1993, tangu Askofu huyo aliposhka madaraka, ameshindwa kusimamia kanisa ikiwa ni pamoja na kuliletea mgawanyiko na kuhujumu mali za kanisa hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.