Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali haikujiandaa vya kutosha kutoa mikopo ya Kikwete
Serikali haikujiandaa vya kutosha kutoa mikopo ya Kikwete
By Habari Tanzania | Published  02/28/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

MABILIONI ya Rais Jakaya Kikwete, yaliyosambazwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini, yameendelea kubakia katika benki mbili za NMB na CRDB kwa miezi kadhaa sasa.

Fedha hizo ambazo tumekuwa tukielezwa kuwa zinalenga kuchochea ujasiriamali miongoni mwa Watanzania ziliahidiwa mapema kabisa na Kikwete mwenyewe, kabla ya kupata baraka za Bunge.

Tangu wakati huo hadi hivi sasa, serikali imekuwa katika hatua mbalimbali za kuziandaa na hatimaye kuzisambaza fedha hizo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Hata hivyo tangu serikali yenyewe itangaze kwa mbwembwe nyingi kuwa fedha hizo, shilingi bilioni moja zilizotengwa kwa ajili ya kila mkoa zilikuwa zimeshafika kote nchini, hakuna mahali ambako watu wameshaanza kupewa kwa ajili ya shughuli hizo zilizokusudiwa.

Jijini Dar es Salaam kwa mfano, wananchi mbalimbali walifikia hatua ya kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa ili kulia hali baada ya jitihada zao za kupata fedha hizo kukwama.

Kikubwa ambacho kimekuwa kikiwakwamisha wananchi hao wengi ni masharti magumu wanayokutana nayo kabla ya kupatiwa mikopo hiyo kutoka katika benki hizo mbili zilizopewa jukumu la kutoa mikopo; CRDB na NMB.

Masharti hayo ambayo taarifa zinaeleza kuwa ni ya kitaalamu, kwa namna moja au nyingine yamekwamisha maamuzi yaliyochukuliwa kisiasa zaidi na serikali kuliko kitaalamu.

Jambo baya katika masharti hayo ni ukweli kwamba, kukosekana kwa mikopo hiyo kumeonekana kuwashtua viongozi wa serikali, na tayari Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chiligati wameshatoa kauli kuhusu suala hilo.

Lowassa ambaye alikuwa akizungumza juzi mjini Morogoro, alizilaumu benki hizo mbili kwa kushindwa kwake kuanza kutoa mikopo hiyo wakati tayari serikali ilikuwa imefikia muafaka na taasisi hizo mbili za fedha.

Katika hoja zake, serikali inasema kwamba, dhamana ya shilingi bilioni 5.3 iliyowekwa katika benki hiyo, inajitosheleza, na kwamba wakopaji hawastahili kukabiliana na masharti mengine tena baada ya hali hiyo.

Hata hivyo, pamoja na dhamana hiyo, benki hizo zimekuwa zikipata shida kuwakopesha wajasiriamali wasio na leseni za biashara, wakulima na wafugaji kutokana na kutofikia taratibu za kawaida za ukopeshaji wa kibenki.

Mvutano uliojitokeza kati ya benki kwa upande mmoja na serikali na wakopaji kwa upande mwingine, unatufundisha jambo moja rahisi, kuwa, kulikuwa hakuna maandalizi ya kutosha yaliyofanywa katika zoezi zima la mikopo hiyo.

Tunaamini kwamba, iwapo kungekuwa na mawasiliano ya kina kati ya benki na serikali, basi hicho kikwazo cha masharti magumu kisingekuwapo katika kipindi hiki.

Kwa sababu ya upungufu huo, ni imani yetu kwamba, serikali itakaa chini na kuuangalia kwa umakini utaratibu mzima wa mikopo hiyo, ili kuufanya uwe wa kudumu na kuwafikia wale waliokusudiwa.

Tunasema hivyo tukitambua kwamba, iwapo zoezi hilo litafanywa kiholela, basi kuna uwezekano mkubwa kwa serikali kujikuta ikikwama kuendelea kutoa mikopo hiyo, hasa kama wakopeshwaji watashindwa kulipa madeni yao na kuingia mitini.

Tunaamini kwamba, mikopo hii ya Kikwete, haiwezi kuifanya serikali ikaja kulazimika kutunga sheria ya kuwafikisha kortini wakopaji watakaoshindwa kulipa kama inavyotaka kufanywa sasa kwa wasomi waliopewa mikopo ya elimu ya juu ambao wengi wao wametokomea pasipo kulipa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by mr njuu)
    Rating
    ni kweli kbs mikopo hii inaonekana imekaa zaidi kisiasa kuliko kiuchumi kwani wanasiasa wanaangalia upande wao tu bila kuandaa mazingira mazuri yatakayowafanya walengwa wairejeshe mikopo yenyewe hasa ukizingatia Watanzania wengi hawana utamaduni wa kulipa madeni.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.