Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  ‘Tumieni Kiswahili kukabili ushindani wa habari’
‘Tumieni Kiswahili kukabili ushindani wa habari’
By Habari Tanzania | Published  02/28/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mustafa Leu

SERIKALI imevitaka vyombo vya habari nchini kutumia kwa usahihi lugha ya Kiswahili ikiwa ni mbinu ya kukabiliana na ushindani uliopo katika soko la habari duniani.

Rai hiyo imetolewa jana mjini hapa na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 85 wa waandaaji wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia redio na televisheni.

Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TUT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Khatib, alisema redio na luninga vinapaswa kuepuka lugha za mitaani, badala yake vihakikishe kuwa vinatumia kwa ufasaha lugha ya Kiswahili kama silaha mojawapo ya kuweza kumudu soko la ushindani katika sekta ya habari.

Alisema, kwa kuwa lugha za mitaani zinazotumika kwa baadhi ya redio zimekuwa haziinufaishi jamii, hivyo zisipewe nafasi.

“Hivi sasa kuna baadhi ya redio zinaruhusu matumizi ya lugha za mitaani, hivyo ni kukiharibu Kiswahili, lugha ambayo tunapaswa kujivunia kwani ni lugha ya bara la Afrika na Tanzania ndio waasisi wake,” alisema Waziri Khatib.

Aidha, aliwataka wadau hao kuandaa vipindi hivyo kitaaluma zaidi na kutumia vibwagizo vitakavyotoa ushawishi kwa wengine kuvisikiliza.

Pia alisema mbali na kuwepo kwa matumizi hayo sahihi, waandaaji hao wanapaswa kuwa na mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi kwa kuwa wote kwa pamoja wakishirikiana wataweza kutimiza lengo la utolewaji wa elimu hiyo kwa umma.

Nae Mkurugenzi wa TUT, Danstan Tido Mhando, alisema mkutano huo umelenga zaidi kuboresha na kuongeza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili na kuanzishwa kwa kituo maalumu cha kuhamasisha matumizi ya lugha hiyo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.