Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Muhimbili yakatiwa umeme
Muhimbili yakatiwa umeme
By Habari Tanzania | Published  02/28/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

MENEJIMENTI ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jana ilijikuta katika wakati mgumu baada Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukata umeme hospitalini hapo.

TANESCO ilifikia hatua hiyo kutokana na malimbikizo ya sh milioni 75 ya ankara za umeme inazoidai hospitali hiyo.

Habari zilizolifikia Tanzania Daima kutoka MNH zilieleza kuwa, umeme ulikatwa jana asubuhi, hali iliyosababisha baadhi ya huduma hospitalini hapo kusitishwa.

Huduma zilizositishwa ni za upasuaji, X-ray na katika wodi zinazotumia mashine za hewa ya oksijeni.

“Kukosekana kwa umeme katika hospitali kubwa kama hii ni aibu kubwa kwa taifa, tunaamini kwamba serikali ilikuwa ikitoa pesa, lakini kutokana na uzembe wa watu wachache deni limekuwa kubwa, tunasikia limefikia sh milioni 100,” kilieleza chanzo hicho cha habari.

Akizungumza na Tanzania Daima kuhusu suala hilo, Meneja Uhusiano wa TANESCO, Daniel Mshana, alisema umeme ulikatwa katika hospitali hiyo jana asubuhi, lakini ulirudishwa majira ya jioni baada ya hospitali hiyo kupeleka hundi ya sh milioni 47.

Mshana alisema baada ya MNH kulipa kiasi hicho cha fedha, TANESCO ilikubali kurudisha huduma ya umeme hospitalini hapo kwa masharti ambayo hata hivyo hakuyataja.

Alisema deni lililobaki, sh milioni 28 linapaswa kulipwa kulingana na mkataba maalumu waliokubaliana, vinginevyo shirika hilo halitasita kukata umeme hospitalini hapo.

Alipotafutwa kwa njia ya siku, Mkurugenzi wa MNH, Prof. Leonard Lema, simu ilikuwa haipatikani.

Habari zilizoifikia Tanzania Daima kabla ya kwenda mitamboni zilieleza kuwa, baada ya umeme kukatwa, jenereta ya hospitali iliwashwa kwa ajili ya kusaidia huduma za dharura.

Hata hivyo, habari zaidi zilieleza kuwa, jenereta hilo halina uwezo wa kumudu kutoa huduma kwa hospitali nzima.

Jana, gazeti hili liliripoti kuwa hali ya mambo katika Hospitali ya Muhimbili si shwari, baada ya menejimenti ya sasa kuanza kufumua kashfa za ulaji wa fedha, uliokuwa ukifanywa na uongozi uliopita.

Kwamba, hatua hiyo imewaweka katika hali ya wasiwasi baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo, waliokuwa na maamuzi makubwa ya matumizi ya fedha katika menejimenti iliyopita.

Uongozi wa hospitali hiyo ulipiga marufuku kuonekana kwa gari la wagonjwa (Ambulance) katika maeneo ya hospitali baada ya kudaiwa kuwa kulikuwepo na mianya ya rushwa katika ununuaji wa gari hilo.

Hatua hiyo ya menejimenti ilipingwa na wakala wa aliyeuza gari hilo, kwa maelezo alipata baraka za kutafuta gari la aina yoyote kutoka katika uongozi uliopita.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.